Taifa Jang’ombe yafungwa 1-0 na Kilimani City

0

Timu ya Taifa Jang’ombe ilishindwa kuonyesha makali yake baada ya kufungwa na timu ya Kilimani city 1-0. Mchezo huo ulichezwa usiku wa Jumatatu Oktoba 17 katika uwanja Amani, Zanzibar.

kilimani city

Na katika matokeo ya mechi nyingine timu Miembeni FC iliwafunga Kimbunga 1-0, vile vile timu ya Mundu ilikubali kucharazwa magoli 3-1 na Kijichi FC. Michezo yote hiyo ilichezwa katika uwanja wa Amani kwa nyakati tofauti.