Taifa Jang’ombe kuchuana na Chuoni nusu fainali Uwanja wa Amani

0

Nusu fainali ya kombe la mtoano kati ya Taifa ya Jangombe dhidi ya Chuoni mchezo huo utapigwa Jumatatu hii ya Oktoba 10 saa 1:00 usiku katika uwanja wa Amaan.

taifa-ya-jangombe

Taifa ya Jangombe walitinga katika hatua hiyo baada ya kuwatoa timu ya New King inayotokea katika Mkoa wa Kazkazini Unguja wakati Chuoni wao waliwatoa timu ya Kijichi.

Nusu fainali nyengine ipo kati ya Mabaharia Weusi timu ya Black Sailors watashindana na Villa United “Mpira Pesa”.

Sailors waliwatoa Robo fainali timu ya Medison wakati Villa wao waliwapiga Miembeni wazee wa Kwalalumpa.