Categories
Videos

New Video: Smile The Genius – Murika

Hii hapa ni video mpya ya msanii Smile The Genius, na kama hujaupata wimbo wake bonyeza hapa. Video ya wimbo huo unaitwa “Murika”, video imetayarishwa na director Creator 5.

Angalia video hiyo na utoe maoni yako.

Categories
Music

New Music: Smile The Genius – Murika

Wimbo mpya kutoka kwa msanii wa kizazi kipya Smile the Genius, wimbo unaitwa “Murika”. Wimbo umetayarishwa na producer Chidy Master.

Sikiliza wimbo huo na utoe maoni yako.

 

Categories
Videos

New Video: Smile ft. Nedy Music – Ti Amo

Smile the genius amewaletea video ya wimbo wake unaitwa “Ti Amo” kama bado hujausikia bonyeza hapa. Katika wimbo huo amemshirikisha Nedy Music.  Video imetayarishwa na director

Categories
Music

New Music: Smile ft. Nedy Music – Ti Amo

Huu ni wimbo mpya kutoka kwa msanii wa muziki Smile unaitwa “Ti Amo” akiwa amemshirikisha Nedy Music. Wimbo umetayaruishwa katika studio za Banny Music na Producer Banny.

Sikiliza wimbo huo na utoe maoni yako.

 

Categories
Videos

New Video: Sharo Music ft. Smile – Nana

Msanii wa muziki Sharo music ameachia video ya wimbo wake mpya unaoitwa ‘Nana’ akiwa amemshirikisha Smile. Video imetayarishwa na Director Panther na Dully Smart.

Angalia hapo na utoe maoni yako

 

Categories
Music

New Music: Smile ft. Sultan King – Toriro

Msanii wa muziki kutoka Zanzibar Smile ameachia wimbo mpya unaoitwa ‘Toriro’ akiwa amemshirikisha Sultan King. Wimbo umetayarishwa katika studio za Jupiter Records na Producer Bonge JR.

Sikiliza Hapa

 

Categories
E! News

Smile na Sultan King kulimaliza bifu lao kwenye ‘Toriro’ Jumatatu hii

Heshima ya muziki wa zanzibar unazidi kupewa nguvu baada ya wasanii wawili kusemekana walikuwa hawakai zizi moja kutokana na uhasama waliokuwa nao watu hao wawili.

Lakini hivi karibuni Smile alionekana kuandika taarifa ambayo ya kushangaza katika ukurasa wake wa Facebook baada ya kuweka cover ya wimbo wake mpya ambao unatarajiwa kuachiwa Jumatatu hii ya Juni 8 na kuonekana ya kuwa ilikuwa ni KIKI ya wimbo mpya.

Wimbo huo unaitwa ‘Toriro’ ambapo Smile amemshirikisha Sultan King na wimbo umetayarishwa na Producer Bonge JR.

Categories
Music

New Music: Sharo Music ft. Smile – Nana

Nakukaribisha kuusikiliza wimbo mpya wa Sharo Music akiwa amemshirikisha Smile. Wimbo umetayarishwa katika studio za Minane Records chini ya producer Bonge Jr.

Sikiliza hapo chini

 

Categories
E! News

Smile atoa majibu kuhusiana na shutuma za Producer Touch juu ya wimbo wa ‘Saa Ngapi’

Msanii wa muziki, Smile ameamua kutokaa kimya kuhusiana na lawama alizotupiwa na mtayarishaji wa muziki Chidy Touch juu ya kutompa taarifa yoyote kuhusiana na wimbo wa Saa Ngapi ambao ulianza kutengenezwa katika studio yake kabla kwenda WCB.

smile

Akiongea na Zenji255, Smile amesema kuwa ni kweli alitengeneza kwake lakini hatotaka litokee tatizo na mtayarishaji huyo na yupo kulimaliza kwani kwa sasa yeye hatopenda kugombana na mtu yoyote kuhusiana na muziki.

“Sitaki beef na mtu kwa sasa” Amesema Simle “Mimi kiupande wangu kuna vingi naweza nikaongea mimi lakini ikawa sio sahihi kwake. Kama wimbo nimeutengeneza muda mrefu na kwanini asizungumze toka mwaka jana wimbo ulipotoka halafu aje kulalamika sasa hivi” Amemalizia Smile.

Categories
E! News

Smile atangaza uongozi wake mpya

Msanii Smile ametangaza rasmi kuhusiana na uongozi wake mpya ambao utakuwa ukimsimamia kazi zake pamoja na maisha yake.

smile

Hitmaker huyo wa wimbo wa ‘Saa Ngapi’ ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Facebook kuwa “Kwa Miaka 5 Sasa Nafanya Game ya Music Tanzania, Kuna baadhi mameneja walijaribu kutaka kunitumia vibaya ila mungu akaniokoa, ukiacha G_Project ambayo ndio uongozi wangu wa kwanza na kunitoa kwenye kiza. Napenda niutangaze uongozi wangu mpya ambao utakuwa unasimamia kazi pamoja na maisha yangu ni Alabama Entertainment” Amesema Smile.

Categories
Music

Music: Smile – Naogopa (Leaked)

Umevujaa!! Jina la wimbo ni ‘Naogopa’ kutoka kwa msanii Smile The Genius. Bonyeza play hapo chini kuusikiliza wimbo huo.

 

 

Categories
E! News

Picha: Smile the genius afunga ndoa

Mkali wa wimbo wa Saa ngapi. Smile The Genius ameingia kwenye list ya mastaa wa Zanzibar waliofunga ndoa mwaka 2016 baada ya kufunga ndoa hapo jana Ijumaa, Disemba 24 na mpenzi wake wa muda mrefu Khuzaima.

“Najisikia poa sana” ameiambia Zenji255 “Especially kuwa na mtu ambaye ana sifa zote za kuitwa mke, mtu ambae ana misingi ya kidini. Allah atuongoze katika hatua hii muhimu na inshallah kwa uwezo wake na dua za ndugu, jamaa na marafiki tutakuwa na ndoa njema yenye upendo na utulivu.” Amesema Smile.

Categories
Videos

New Video: Smile – Saa Ngapi

Msanii Smile ameachia video yake  mpya ‘Saa Ngapi’. Video imetayarishwa na Director Kenny.

 

Categories
E! News

Smile na I.T waamua kuzungumza kuhusiana na ugomvi uliokuwepo kati yao

Kwa mbio za wasanii wa Zanzibar na mwendo wanaoenda nao hivi sasa muziki wa Zanzibar unaweza ukaelekea pahala sio pazuri.

ugomvi

Ugomvi kati ya msanii na msanii kiupande mwingine haiwezi kusaidia muziki wa jamii fulani kukaa katika sehemu nzuri na yenye kuleta manufaa japokuwa wengine husema itaweza kumpa umaarufu msanii kwani kila wakati atakuwa anatajwa jina lake kutokana tukio husika lililomkuta.

Nadhani kwa Zanzibar ni muda mrefu wasanii wa Zanzibar wanajitahidi kila siku kuliweka soko lao la muziki Zanzibar likae katika (level) muelekeo mzuri lakini inashindikana kutokana na chuki, ubinafsi pamoja na kutokuwa na umoja. Na ni nini kinasababisha haya?

Zenji255  ilikaa chini na kuongea na wasanii wa muziki wa kizazi kipya I.T na Smile kwa nyakati tofauti ambapo hivi karibuni walionekana kutoelewana huku wakirushiana maneno kupitia mitandao ya kijamii.

I.TMsanii I.T alisema kuwa kwa upande wake hajawahi kugombana na mtu yoyote kwani huenda ikachangia muziki na maisha yake yakakaa sehemu mbaya kwani ugomvi huenda ukasababisha chuki.

“Mimi ninachoshangaa Smile nikikutana nae naona haniambii lolote kama kuna kitu nimemkwaza ama la, naona tunasalimiana vizuri. Kwanza, Smile anatakiwa afahamu kwamba mimi ni mkongwe wa muziki na mimi siwezi kushindana na watoto wadogo kama yeye anatafuta ‘kiki’ kwa sababu ya wimbo wake una mapungufu kwahiyo akitumia jina langu anaweza akaupatia umaarufu, muziki hauendi kinamna hiyo” Amesema I.T

I.T Alimalizia kiupande kuwa “Ninachomshauri Smile afanye kazi na aandike mashairi mazuri basi atafanya vizuri asiwe na wivu na mafanikio yangu kama ndio kinachomuumiza.”

smile

Na Smile nae amesema kuwa alishawahi onana na I.T na hakuona dalili yoyote na kwake yeye anamuheshimu kutokana I.T kuwepo katika muziki katika kipindi kirefu.

Amesema  Smile “Mimi kwa sasa siwezi nikafikiria kugombana kuhusiana na wasanii wa Zanzibar kwa sababu kila mtu anafanya muziki wake. I.T namfahamu ni mkongwe hapa Zanzibar na vile vile mimi na yeye, yeye yupo kwa kipindi kirefu na anafahamu mambo mengi kuhusiana na muziki wetu lakini kwanini aniongelee mimi mtoto mdogo niliyeanza juzi.”

“Nimekaa mwaka mzima sijaaachia hata wimbo mmoja lakini baada kuachia ‘Saa Ngapi’ nimeanza kuongelewa kwa ubaya. Mimi siwezi nikatafuta kiki kupitia kwake yeye kuna wasanii kibao ninawafikiria kama Diamond, Ali Kiba na Rayvanny, ambao wana mafanikio makubwa katika muziki na yananiumiza  kichwa kila siku ili kuwa kama wao ni sio kama I.T” Ameongea Smile.

Categories
E! News

Smile aongea kisa cha ‘Saa Ngapi’ kilimtokea baada ya kuwekwa maboya

Hitmaker wa ‘Saa Ngapi’ Smile aliamua kuongea ukweli kutokana na wimbo wake huo mpya aliouachia hivi karibuni kuwa ni jambo ambalo lilimtokea yeye mwenyewe.

smile

Akiongea na Zenji255 Smile amesema kuwa miaka mitatu iliyopita ikiwa nyimbo yake ya kichefu chefu inafanya vizuri katika vituo vya TV na redio, lilimtokea jambo hilo akiwa anamsubiri mpenzi wake na matokeo yake hakuweza kutokea.

“Wazo la ‘Saa Ngapi’ nilikuwa ninalo miaka mingi lishawahi kunipa adabu mimi mwenyewe nilipowekwa maboya na mpenzi wangu wa zamani ambapo alipanga tuonane ila hakutokea.” Amesema “Na nilikuja kugundua kuwa sio peke yangu tu duniani pia matatizo kama haya yashawakuta wengi aidha mwanamke au mwanamme.” Aliongeza Smile.

Categories
Music

Music: Smile & Abramy – Salome (Cover)

Wasani wa kizazi kipya Smile na Abramy wafanya cover ya wimbo wa Diamond Platnumz alioshirikiana na Rayvanny ‘Salome’.

Sikiliza hapa

 

Categories
Music

New Music: Smile – Saa Ngapi

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Smile ameachia wimbo wake mpya ‘Saa Ngapi’. Wimbo umetengenezwa katika studio za Wasafi chini ya Producer Lizer Classic

Sikiliza hapa na usisahau kuacha maoni yako hapo chini.

 

Categories
E! News

Audio: Smile aelezea ukimya wake ulivyozaa matunda ya nyimbo 4 katika studio za WASAFI

Msanii Smile anatarajia kuuvunja ukimya wake wa muda mrefu miezi ya hivi karibuni kuanzia sasa kwa kuachia moja kati ya nyimbo zake mpya ambazo alizorekodi katika studio za WASAFI.

smileAkiongea na Zenji255 Jumapili hii Smile alisema zipo nyimbo nyingine alizofanya katika studio tofauti za Dar na Zanzibarili kuukuza muziki wake kibiashara zaid.

Msikilize Smile Akizungumza na Mkali Nesta

Categories
Videos

#TBT: Smile – Kichefuchefu (+Video)

Ni miaka minne sasa tangu msanii kutokea Zanzibar Smile kuachia wimbo wake wa kwanza ambao uliomtambulisha katika tasnia ya muziki wimbo wa ‘Kichefuchefu’. Wimbo huu umetengenezwa katika studio za Uprise Music chini ya Producer Fraga na video imeongozwa na Adam Juma.

Tupia maoni yako hapa.

 

Categories
Music

New Music: Mubacriss ft. Smile – Haufanani

Msanii Mubacriss kutoka Zanzibar ameachia wimbo wake mpya ‘Haufanani’ akiwa amemshirikisha Smile. Wimbo umetayarishwa na Producer Bab Chidy katika studio Island Records Zanzibar.