Categories
E! News

Lumi aiomba serikali ipiganie vituo vya redio kucheza muziki wa Zanzibar kwa 90%

Mtayarishaji kutoka studio za Mandevu, Lumi ameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipiganie katika kusimamia kazi za wasanii wa Zanzibar kuchezwa katika vituo vya redio vya hapa kwa asilimia 90.

lumiAkiongea na Zenji255 Lumi amesema kuwa sio wanamuziki wengi wanaitaka studio ya serikali kufanya kazi zao za muziki, bali wengi wanataka serikali inahakikisha inasimamia kazi za wasanii wa muziki kwa kutoa amri kwa vituo vya redio kazi zao ziwe zinachezwa bure na bila pingamizi ya kutaka hongo.

“Serikali lazima iweke mkazo” Lumi amesema “Unakuta DJ mwanzo wa kipindi mpaka mwisho hajagusa hata kidogo wimbo wa msanii wa Zanzibar, halafu mwisho wa siku DJ ana shida anataka msanii amsaidie. Kwanini asimtafute Davido au Diamond akamwambia kwamba nimecheza wimbo wako wiki nzima kwahiyo nisaidie kiasi fulani nina shida, tuone kama atakusaidia” Amesema Lumi.

Categories
E! News

‘Nilishawahi sema mbele ya viongozi lakini serikali bado haijaamua kuusaidia muziki wa Zanzibar’ – Lumi

Mtayarishaji wa muziki kutoka studio za Mandevu records, Lumi amesema alishawahi kutamka maneno ya kuwapa ushauri viongozi wa serikali kuhusiana na kuusaidia muziki wa Zanzibar kukua lakini mpaka sasa bado shauri hilo halijafanyiwa kazi.

slim

Akiongea na Zenji255 Lumi amesema kuwa serikali bado haijawa tayari kuusaidia muziki wa Zanzibar na ndio maana wasanii wengi huwa wanavilalamikia vyombo vya habari na wengine kukimbilia kwenye mambo yasiyofaa.

“Mcheza kwao hutunzwa, na sisi hatuwezi kuwatunza watangazaji ambao hawausaidii muziki wetu” Ameongea Lumi. “Huwezi kusema muziki ni Ajira wakati hakuna msaada wowote unaopata kuanzia vyombo vya habari mpaka serikali husika. Ukienda kwenye maredio msanii anatakiwa kulipa ili wimbo wake uchezwe wakati kina Davido hata shilingi hawatoi na nyimbo zao zinachezwa.” Amesema Lumi