Categories
Z! Extra

Barrack Obama akosoa viongozi wenye kutoa kauli za kibaguzi na chuki

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama amewataka Wamarekani kukataa lugha za chuki na kibaguzi kutoka kwa viongozi wao.

Obama amekuwa akiongea kwa nadra tangu alipoondoka madarakani, na japo hakumtaja kiongozi yeyote kwa jina, lakini kauli yake hiyo imekuja baada ya rais Donald Trump akiwa katika harakati za kujinasua kuwa kauli zake dhidi ya wahamiaji ndizo chanzo cha kuchochea mauaji nchini humo.

Katika hotuba yake jana Jumatatu, Trump alikemea ubaguzi wa rangi. Jumla ya watu 31 wameuawa katika mashambulio ya bubduki kwenye majimbo ya Texas na Ohio mwishoni mwa wiki.

 

Akiwa madarakani, Obama alipigana pasi na mafanikio kudhibiti umiliki wa silaha za moto nchini Marekani. Aliiambia BBC mwaka 2015 kuwa, kushindwa kupitisha kwa sheria za kudhibiti silaha ndilo jambo kubwa alilofeli akiwa kama kiongozi wa nchi hiyo.

Trump kulipa kisasi kwa ”upumbavu”wa Macron Mkuu wa ujasusi Marekani ajitenga na utawala wa Trump. Obama amekuwa akikwepa kuzungumzia sera za Trump, hususani ya uhamiaji ambayo imekuwa ikipingwa na makundi tofaouti, hata hivyo, safari hii ametoa tamko.

“Inabidi kwa pamoja tukatae lugha zinazotoka kwenye kinywa cha kiongozi wetu yoyote ambaye analisha mazingira ya uoga na chuki ama anayefanya ubaguzi kuwa jambo la kawaida. Viongozi ambao wanawafanya watu ambao hawafanani nasi kuonekana kama mashetani, ama wanaodai kuwa watu wengine ikiwemo wahamiaji wanahatarisha mfumo wetu wa maisha, ama wanaodai kuwa Marekani ni ya jamii moja tu ya watu,” amesema Obama.

Categories
Music

#TBT: N.I – Nakwita (+Music)

Ni #ThrowBackThursday na kujikumbusha. Kwa Upande wa muziki, msanii aliyekua anaunda kundi la Bz Broo kutoka Michenzani Zanzibar, N.I alishawahi kuwa kama ‘solo artist’ na kuachia wimbo wake wa kwanza unaitwa ‘Nakwita’ wimbo umetayarishwa katika studio za Akhenaton Records na producer Lil Ghetto.

Jikumbushie kitambo hicho kwa kusikiliza muziki kutoka kwa N.I

Categories
E! News

Hii hapa ni ‘suprise’ nyingine kutoka kwa Chidy Grenade ambayo huenda ikaachiwa karibuni

Wiki kadhaa zilizopita Zenji255 ilishawahi toa maoni juu ya wasanii chipukizi ambao watakaofanya vizuri kwa mwaka 2017 na kuweza kuutangaza muziki mbali zaidi, Chidy Grenade hivi karibuni amefunguka kuhusiana na ujio wake mpya ambao huenda akauachia hivi karibuni.

chidy

Akiongea na Zenji255 Chidy amesema kuwa alikua na ndoto kubwa sana katika muziki kukutana na mtayarishaji ambae alikuwa na hamu ya kufanya nae kazi katika muziki wake.

“Nahreel ndie mtayarishaji niliekuwa na-wish kufanya nae kazi” Amesema Chidy Grenade “Na tayari tushafanya hiyo kazi ila kwa sasa siwezi kusema nitaachia lini na wapi kwa ni suprise kwa mashabiki, kutokana na uongozi bado unafanya mipango mingine kabisa ambayo hata haiendani na kazi hiyo iliyokuwepo kwa Nahreel” Amemalizia Chidy Grenade.

Categories
E! News

Pozi Adim kuufungua mwaka na collabo mpya na Sultan King

Baada ya kimya kirefu ambacho alichokuwa akijiweka sawa, msanii wa muziki Pozi Adim jumatatu ijayo anatarajia kuachia wimbo wake mpya akiwa amemshirikisha Sultan King.

pozi adim

Pozi Adim alikuwa kimya kwa muda wa mwaka mzima sasa toka alivyoachia wimbo wake wa msobe msobe mnamo mwezi Machi mwaka 2016, ameamua kuusimamisha ukimya huo kwa wimbo huo mpya.

Akiongea na Zenji255 meneja wa Pozi Adim, Khamis Hk amesema “Wimbo upo tayari tunamalizia michakato ya mwishoni na tuanze ‘Media Tour’ za usambazaji katika vituo vyote vya redio hapa Zanzibar. Wimbo umetayarishwa katika studio za Island records na producer Aloneym”

Categories
E! News

Lady Gaga kuichukua nafasi ya Beyonce onyesho la Coachella

Tamasha la Coachella ambalo linaingiza fedha nyingi zaidi duniani linalofanyika kila mwaka nchini Marekani, baada ya mwanamuziki Beyonce kusitisha onyesho lake katika tamasha hilo sasa limeamua kumueka Lady Gaga ashikilie nafasi hiyo.

lady gaga

Kwa mujibu wa BillBoard, Lady gaga atafanya onyesho lake katika tamasha hilo baada Beyonce kughairi kutokana na kuwa mjamzito wa watoto mapacha.

Lady Gaga hivi karibuni alionekana kufanya vizuri katika show yake aliyofanya katika kipindi cha mapumziko katika mchezo wa Super Bowl na imeelezwa kuwa Lady Gaga atafanya jumamosi mbili (April 15 na 22) katika uwanja wa Polo jijini California.

Categories
E! News

Hizi hapa ni sera 3 endapo Ison Mistari atapewa nafasi ya kugombania urais

Kila binadamu huwa na ndoto kubwa zinazoweza kusaidia kuleta mafanikio kwa njia moja ama nyingine ili kuweza kujikwamua na umaskini. Kwa rapa Ison Mistari amefunguka na sera 3 endapo yeye atakapo kuwa mwanasiasa na kupata nafasi ya kugombania urais atasimamia nini?

Ison

Ison Mistari amesema kwa upande wake hatotaka kabisa kujiingiza katika mambo ya siasa ila ametoa mifano endapo atapewa nafasi hiyo.

Haya hapa ni mambo 3 endapo Ison Mistari akipewa nafasi ya kugombani urais atahakikisha kuyafanya.

  1. Kuwarahisishia watu mzunguko wa pesa kuwa mwepesi

Kwa sasa kwa upande wa Zanzibar mzunguko wa pesa umekuwa mdogo na sio kama vile zamani kulivyokuwa na bandari huru. Biashara zilikuwa nyingi mpaka inafikia hatua wageni mbali mbali kutoka Comorro, Tanga, Mombasa na Dar es Salaam walikuwa wakifika Zanzibar kufanya biashara pakiwa ni kituo kikuu cha biashara maarufu kama ‘Used’.

2. Kulirudisha soko la muziki Zanzibar

Soko la muziki kwa Zanzibar kwa sasa lishaibiwa na halipo tena, wasanii tunahangaika na hatujui tutaupeleka wapi muziki wetu, zaidi ya kuishia maredioni na kuzihifadhi CD zetu majumbani. Zanzibar ilikuwa ndio sehemu ya kwanza kuanzishwa kwa muziki wa kizazi kipya, wasanii wa bongo kama Kwanza Unit walikuwa wanakuja Zanzibar kushoot na kutengeneza nyimbo zao. Mimi nilikuwa katika kundi linaitwa Wanduza Family na tulishawahi kuuza nyimbo zetu katika maduka kama vile Alakeyfak na tulifaidika kwa mauzo yale kwa kipindi kile, lakini sasa hivi hakuna pa kuuza.

3. Kuwapa fursa wawekezaji wote kuwekeza katika soka la Zanzibar

Soka la Zanzibar linazidi kwenda chini siku hadi siku, na hii yote ni baada ya kukosa wadhamini katika soka. Wawekezaji wameekewa vikwazo kwamba kampuni za pombe haziruhusiwi kudhamini soka letu lakini, Bar bado ziko wazi, Kwenye luninga matangazo ya pombe kila siku yanaonyeshwa, watoto wadogo siku hizi wanakunywa pombe tena hadharani. Inatubidi tubadilike na tuangalie wapi tunaweza kusaidia juu ya hili, hata kama sio lazima hao wadhamini wa pombe lakini kama serikali tunao uwezo wa kupata wadhamini wakubwa wa kuliendesha soka letu la Zanzibar.

Categories
E! News

‘Wosia wangu kwa Baraza la Sanaa Zanzibar’ – Khamis HK

Mwanaharakati na meneja anaesimamia wasanii wa muziki wa Zenji Fleva, Khamis HK a.k.a Kaka Meneja, kupitia ukurasa wake Instagram ameamua kutoa wosia wake kwa Baraza la Sanaa la Znazibar. Usome Hapa:

Kwa Baraza la Sanaa la Zanzibar,

Kama Hatutarekebisha hizi Sheria na Kuzisimamia ipasavyo, itafika Mahali Wasanii (Music na Filamu) Watapotea na Hatutakua na wakumlaumu zaid ya sisi wenyewe, ”Kwa sababu” Kwa hali inavyo kwenda sasa hivi, itafika Mahali Wasanii wetu Watakutana Na Msongo wa Mawazo mkubwa kwenye maisha yao, Kwa sababu Kadri wanavyo kua kiumri na miaka..

Wanazidi pia kukabiliana na Majukum zaid ya Kimaisha, na ikafika mahali Wamekua Maarufu saana na Wakashindwa ku afford Kujikim na Maisha yao na familia zao, licha ya wanavyo jitahidi Kujituma Sasa, Hasa ukizingatia Familia Zetu nyingi ni Tegemezi, Wakishindwa kufaidika apo ni Lazima Watapoteza Muelekeo, Nakujikuta Wanaingia kwenye Majanga Mbali mbali Yasio faa kwa Msongo wa Mawazo..

TUJITAHIDINI MAPEMA,KWA SOTE KUTENGENEZA MAZINGIRA YA SANAA KUA AJIRA YENYE KUTEGEMEWA KABLA HAYAJATOKEA HAYA; NI JUKUMU LETU SOTE lakini (BARAZA LA SANAA NDIO WALEZI WA WASANII WANAPASWA KUFANYA JAMBO LA HARAKA MNO). By Khamis Hk (KakaMeneja)🎤🎻🎤

Categories
E! News

Nick Cannon na mchumba wake wapata mtoto wa kiume

Hongera nyingi zinaenda kwa Nick Cannon na mchumba wake Britanny Bell ambapo mnamo Feb. 21, Brittany Bell amejifungua mtoto wa kiume na kumpa jina Golden ‘Sagon’ Cannon.

Mtangazaji huyo wa kipindi cha luninga cha “Wild ‘N Out” amesherehekea taarifa hiyo baada ya kuweka picha katika ukurasa wake wa Instagram akiwa amemshikilia mwanawe  na kuandika:

“Weeping may endure for a night, but Joy cometh in the morning, No matter how hard the world may hit you, God always reminds us of our purpose! #TrueHappiness Welcome to Earth Son!”

Golden Cannon atakuwa ni mtoto wa tatu kwa Nick Cannon ambapo tayari alishazaa na ex wake Mariah Carey watoto mapacha wawili wenye umri wa miaka mitano, Moroccan na Monroe.

Categories
E! News

Nassir Vanillah atarajia kuzindua wimbo na video mpya wikiendi hii

Msanii wa muziki Nassir Vanillah, kwa muda mrefu mashabiki walikuwa katika mkao wa kula wakisubiri ujio wa wimbo wake mpya ‘Najuta Kuoa’ ambao uliotakiwa kuachiwa mwaka jana mwishoni na matokeo yake kubadili mawazo na kuja na wimbo mwingine.

nassir

Akiongea na Zenji255 Nassir, ambaye siku ya Jumamosi (Feb. 25) anatarajia kuzindua wimbo na video yake mpya unaoitwa ‘Biringe Baikoko’ amesema wazo la wimbo wa Najuta kuoa bado lipo ila amefikiria kulisogeza mbele na atauachia baada ya wimbo huu wa sasa kuuachia.

“Kwa sasa najuta kuoa itasubiri kidogo” Amesema Nassir Vanillah “Biringe Baikoko ndio wimbo ambao utakaoruka hewani, na tayari video na wimbo wenyewe upo ambapo tarehe 25 tunauzindua Intebe. Wimbo na video umesimamiwa katika studio  za Tiffu Records na D. Sam ndie aliyehusika katika matayarisho ya video na wimbo wenyewe” Amesema Nassir Vanillah.

Categories
E! News

Chris Brown aongea kuhusiana na kesi aliyofunguliwa na Karrueche, pambano dhidi ya Soulja Boy

Baada ya kukabiliwa na mashtaka pamoja na maneno mengi katika mitandao, ambapo rapa Soulja Boy kudai kuwa Chris Brown anaogopa kupigana nae pamoja na ex wake, Karrueche kumfungulia mashtaka ya kumtishia kumfanyia vurugu na kifo.

chris brown

Chris kupitia ukurasa wa Instagram ameandika: “Make sure y’all don’t be listening to all this b*****, man,” Amesema katika video ya Instagram. “Whatever people on the other side doing, let them do what they doing. I don’t know what the f*** they talking about.”

Kauli ya madai kwa Karrueche ilitoka punde baada ya kushtaki na Chris Brown kuamriwa kuwa akae mbali ya yadi kutoka kwa Karrueche, kaka yake na mama yake mzazi. Katika maelezo aliyoyatoa mahakamani, Karrueche alieleza kuwa Chris alimtishia kumuua kwa kutumia bastola. Na alisema pia Chris alishawahi mpiga na kumsukuma na kuanguka kwenye ngazi miaka kadhaa iliyopita.

Categories
E! News

Watafutaji waelezea mipango inayofuata baada ya ‘Changamoto’ kuachiwa

Kundi la muziki la ‘Watafutaji’ linaloundwa na marapa wawili Buyubaya Mtabiri na Huza B, wamezungumza kuhusiana na mipango yao inayofuata baada ya wimbo wao mpya unaoitwa ‘Changamoto’ siku kadhaa zilizopita.

watafutaji

Akiongea na Zenji255 mmoja wa marapa wa kundi hilo, Huza B amesema kuwa tayari washatengenezea wimbo mwingine na upo katika maandalizi ya mwishoni ila hawapo tayari kuuachia kwani ni mapema sana.

“Tulichojipanga kukifanya kwa sasa tunaanda video ya Changamoto wakati tukiwa tunaendelea na Media tour kwani bado hatujaupeleka wimbo wetu baadhi ya mikoa hapa Tanzania hasa hasa Dar es Salaam. Na mipango kede kede ambayo ni ‘suprise’ kwa mashibiki wetu ipo njiani inakuja na tukijaaliwa tutawajulisha ikiwa tayari” Amesema Huzza B.

Categories
E! News

Picha: New Money ashoot video ya wimbo wake mpya

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Zanzibar, New Money hivi karibuni walionekana wakiwa katika maeneo tofauti wakishoot video ya wimbo wake mpya ‘Nini Tatizo’ alioshirikisha Sultan King na Shareezy.

Akiongea na Zenji255 New Money amesema kuwa ameamua kufanya video hiyo ni baada ya kipindi kirefu alikuwa akiachia wimbo bila ya video, na kuwafanya mashabiki wake kutofurahia jambo hilo juu ya muziki wake.

“Kinachofuata kwa sasa ni kutekeleza mahitaji yanayotakiwa kufanywa kama mwanamuziki kwa mashabiki wake, na tayari tushamaliza mipango yote ya video hivi sasa ndio inaenda kufanyiwa kazi na karibuni tu tutawapa utamu wa video yangu mpya” Amesema New Money.

 

Categories
E! News

Mshindi wa Free Style Chiby K aingia studio kurekodi wimbo wake mpya

Mshindi wa shindano la Run The Beat Free styke Battle, Chiby K ameonekana hapo jana Jumatatu katika studio za Mandevu records akitayarisha wimbo mpya ikiwa kama ni moja ya makubaliano kwa mshindi wa shindano hilo.

Chiby K (Kulia) akiwa na Mtayarishaji wa Mandevu records, Buju (katikati) pamoja na MC Kudo (Kushoto)

Hivi karibuni Chiby K aliibuka mshindi wa shindano hilo baada ya kumbwaga mpinzani wake ‘Devil’ ambaye aliyetoka nae toka awamu ya mwanzo na kumshinda katika hatua ya fainali. Ambapo mshindi anajipatia nafasi ya kurekodi wimbo mmoja kutoka studio ya Mandevu na Video moja kutoka kwa director Huruma.

chiby k

Akiongea na Zenji255, Chiby K amesema kuwa nafasi aliyoshinda ataitendea haki kuanzia wimbo hadi video kwani anataka kudhihirisha kama yeye kweli alikuwa ni mshindi mstahiki katika mashindano hayo.

“Wimbo ndio tayari upo jikoni unaanza kuwekwa viungo na mambo mengine, vile vile mipango ya video itafuata baada ya mimi kuwa tayari nishaweka sauti na kila kitu halafu kabla ya wimbo kuisha nitachukua demo kwa ajili ya kurekodi video na baadae wimbo utawekwa ukiwa tayari, cha zaidi ninachowaomba mashabiki wa muziki wanipokee kijana wao Chiby K Solja” Amesema Chiby K

Categories
E! News

Mfahamu Lady Black: Rapa wa kike pekee kutoka Zanzibar aliyevutiwa na Sista P

Katika kiwanda cha muziki ambacho kina rappers wa kike wachache kutoka Zanzibar, Lady Black kwa kipindi kirefu alikuwa kimya na sasa amerudi tena rasmi baada ya kuonekana studio za Action records akiwa anaanda midundo mipya kutoka studio hapo.

Lady Black akitoa free style katika show ya mualiko wa chama cha wasanii wa muziki wa kizazi kipya iliyofanyika Coco Blue – Jambiani.

Huenda ukawa unamfahamu juu juu tu, mfaham zaidi.

Kwa jina kamili anaitwa Felista Philipo Magindo a.k.a Lady Black kwa sasa makazi yake ni Zanzibar, alianza sanaa ya muziki wa rap miaka saba iliyopita ambapo alikuwa akirap akiwa kwenye Ma-Camp (kwenye mkusanyiko). Kwa kipindi hicho alikuwa bado hajapata nafasi ya kuingia studio kwani kwa upande wake anasema hali ilikuwa ngumu kwenda studio.

“Yaani katika huwezi kuamini nilianza kuingia studio miaka miwili iliyopita katika saba ya muziki wangu. Na wasanii walionivutia zaidi na kunifanya mpaka nikaupenda muziki hasa hasa rap: Sista P, Zay B na Witness. Na kwa sasa tayari nilishaachia nyimbo 2, na nyingine tayari ipo jikoni inasimamiwa na producer Chilly K wa Action records” Amesema Lady Black.

Ameongeza kuwa katika kilichokuwa kinamfurahisha katika muziki na sehemu aliyokuwa anaishi Kigamboni, kulikuwa na ushindani mkubwa wa ma-Camp ambapo wanashindanishwa kurap (Free style Battle) na yeye ndipo akaamua kujiingiza katika mashindano lakini hakufanikiwa kushinda ila haikumfanya akate tamaa kwenye rap.

“Kwa kweli bado natamani mashindano yale ya ma-Camp yarudi tena hata huku Zanzibar  yawe yanafanyika kila mwezi au kila baada ya miezi kadhaa yafanyike sababu yanaibua vipaji vingi ila watu hawajui” Amemalizia Lady Black.

Categories
E! News

Picha: Ison alivyotoa burudani katika Usiku wa Tamaduni Muzik

Show ya Tamaduni iliyofanyika Jumamosi hii katika viwanja vya Kilinge jijini Dar es salaam ilikuwa ni show ya aina yake ambapo ilishirikisha marapa mbali mbali kutoka jijini akiwemo na rapa Ison Mistari ambaye alipata mualiko kuonyesha makali yake.

Show hiyo ilikuwa maalum kwa wasanii wanaotokea katika lebo hiyo na wanaofanya muziki aina Hip Hop ambapo alionekana rapa kama One the Incredible pamoja aliambatana na timu nzima ya Stone Town records.

Angalia picha za show hiyo ilivyokuwa

Dj Walid kutoka Stone Town Records
Ison akiwa jukwaa moja na One The Incredible

Categories
E! News

Alatish Mabawa kumtambulisha ‘Twarity’ na wimbo wake mpya Jumatatu ijayo

Msanii wa muziki Alatish Mabawa kupitia lebo yake ya ‘Mabawa Classic’ Feb 20 atamtambulisha rasmi msanii mpya ‘Twarity’ ambaye tayari ameshatengeneza wimbo mpya unaoitwa ‘Kipenda Roho’ ambao ameshirikishwa Mabawa.

alatish mabawa

Akiongea na Zenji255, Mabawa amesema kuwa hadi sasa tayari ameshasaini msanii mmoja na bado na mipango ya kuwasaini wengine ambao watakuja kutangazwa siku za mbele.

Kwa upande wake amesema kuwa amechukua uamuzi huo baada ya kuona vipaji Zanzibar vinaibuka vipya kila siku.

“Zanzibar vipaji vipo vingi tu ila msaada wa kuvinyanyua ni mdogokuna wasanii wazuri mtaani. Nimeamua kuanzisha lebo ili kuwasaidia wasanii wenye vipaji kuonyesha uwezo wao, kupitia lebo yangu nataka kuleta mapinduzi. Na bado nina mipango mingine tofauti na muziki katika kuendeleza vipaji vipya vya hapa Zanzibar” Amesema Mabawa

Wimbo wa msanii Twarity umetengenezwa katika studio za Six Records na producer Side to The Lee akiwa pamoja na Chilly K.

Categories
E! News

‘Tuna mipago ya kufanya kolabo na msanii wa Zanzibar’ – H_art The Band

Kama utakuwa unaukumbuka wimbo wa ‘Uliza Kiatu (Ask My shoes)’ wa kundi la H_art The Band kutoka Kenya, hivi karibuni wamesema wana mipango wakirudi tena Zanzibar wafanye kolabo na baadhi ya wasanii ili kupata ladha tofauti katika muziki wao.

h_art the band

Akiongea na Zenji255, mmoja wa wanaounda kundi hilo Ken, amesema kuwa ni mara yao ya kwanza kufika Zanzibar lakini vitu ambavyo walivyokutana navyo kuanzia sanaa ya muziki mpaka uchoraji, uchongaji na nyinginezo zimewavutia na kufikiria kufanya kitu ambacho kinaendana na muziki wao.

“Unajua sisi aina yetu ya muziki tunayofanya ni Afro-Poetry, ni muziki wa kiafrika uliochanganywa na mashairi ndani. Na kwa upande wa Zanzibar tumeona aina ile ile inayoendana na muziki wetu kama vile Taarab, ambayo mashairi yake na muziki ukisikiliza ni ya ndani kwa ndani. Mipango ikiwa sawa tutarudi kufanya kolabo na wasanii wa huku. Sio Taarab tu, hata aina yoyote ya muziki unaopatikana Zanzibar” Amesema Ken.

Categories
E! News

Hii hapa ni orodha ya washindi wa tuzo za 59 za Grammy

Mastaa mbali mbali nchini walikaa pamoja na kushuhudia uchukuaji wa tuzo za awamu ya 59 za Grammy zilizofanyika katika ukumbi wa Staples Center jijini Los Angeles usiku wa Jumapili (Feb. 12).

grammy

Katika tuzo hizo mwanadada Adele aliweza kuondoka na tuzo 5 usiku huo zikiwemo tuzo 3 kubwa za Wimbo, Rekodi na Albamu bora ya mwaka. Huku Chance the Rapper alishinda tuzo chipukizi wa mwaka.

Isome orodha ya washindi hapo chini

RECORD OF THE YEAR
“Hello” – Adele
“Formation” – Beyoncé
“7 Years” – Lukas Graham
“Work” – Rihanna Featuring Drake
“Stressed Out” – Twenty One Pilots

ALBUM OF THE YEAR
25 – Adele
Lemonade – Beyoncé
Purpose – Justin Bieber
Views – Drake
A Sailor’s Guide To Earth – Sturgill Simpson

SONG OF THE YEAR
“Formation” – Khalif Brown, Asheton Hogan, Beyoncé Knowles & Michael L. Williams II, songwriters (Beyoncé)
“Hello” – Adele Adkins & Greg Kurstin, songwriters (Adele)
“I Took A Pill In Ibiza” – Mike Posner, songwriter (Mike Posner)
“Love Yourself” – Justin Bieber, Benjamin Levin & Ed Sheeran, songwriters (Justin Bieber)
“7 Years” – Lukas Forchhammer, Stefan Forrest, Morten Pilegaard & Morten Ristorp, songwriters (Lukas Graham)

BEST NEW ARTIST
Kelsea Ballerini
The Chainsmokers
Chance The Rapper
Maren Morris
Anderson .Paak

BEST POP SOLO PERFORMANCE
“Hello” – Adele
“Hold Up” – Beyoncé
“Love Yourself” – Justin Bieber
“Piece by Piece (Idol Version)” – Kelly Clarkson
“Dangerous Woman” – Ariana Grande

BEST POP DUO/GROUP PERFORMANCE
“Closer” – The Chainsmokers Featuring Halsey
“7 Years” – Lukas Graham
“Work” – Rihanna Featuring Drake
“Cheap Thrills” – Sia Featuring Sean Paul
“Stressed Out” – Twenty One Pilots

BEST POP VOCAL ALBUM
25 – Adele
Purpose – Justin Bieber
Dangerous Woman – Ariana Grande
Confident – Demi Lovato
This Is Acting – Sia

BEST DANCE RECORDING
“Tearing Me Up” – Bob Moses
“Don’t Let Me Down” – The Chainsmokers Featuring Daya
“Never Be Like You” – Flume Featuring Kai
“Rinse & Repeat” – Riton Featuring Kah-Lo
“Drinkee” – Sofi Tukker

BEST DANCE/ELECTRONIC ALBUM
Skin – Flume
Electronica 1: The Time Machine – Jean-Michel Jarre
Epoch – Tycho
Barbara Barbara, We Face A Shining Future – Underworld
Louie Vega Starring…XXVIII – Louie Vega

BEST ROCK PERFORMANCE
“Joe (Live From Austin City Limits)” – Alabama Shakes
“Don’t Hurt Yourself” – Beyoncé Featuring Jack White
“Blackstar” – David Bowie
“The Sound Of Silence (Live On Conan)” – Disturbed
“Heathens” – Twenty One Pilots

BEST R&B PERFORMANCE
“Turnin’ Me Up” – BJ The Chicago Kid
“Permission” – Ro James
“I Do” – Musiq Soulchild
“Needed Me” – Rihanna
“Cranes In The Sky” – Solange

BEST TRADITIONAL R&B PERFORMANCE
“The Three Of Me” – William Bell
“Woman’s World” – BJ The Chicago Kid
“Sleeping With The One I Love” – Fantasia
“Angel” – Lalah Hathaway
“Can’t Wait” – Jill Scott

BEST R&B SONG
“Come See Me” – PartyNextDoor Featuring Drake
“Exchange” – Bryson Tiller
“Kiss It Better” – Rihanna
“Lake By The Ocean” – Maxwell
“Luv” – Tory Lanez

BEST URBAN CONTEMPORARY ALBUM
Lemonade – Beyoncé
Ology – Gallant
We Are King – KING
Malibu – Anderson .Paak
Anti – Rihanna

BEST R&B ALBUM
In My Mind – BJ The Chicago Kid
Lalah Hathaway Live – Lalah Hathaway
Velvet Portraits – Terrace Martin
Healing Season – Mint Condition
Smoove Jones – Mya

BEST RAP PERFORMANCE
“No Problem” – Chance The Rapper Featuring Lil Wayne & 2 Chainz
“Panda” -Desiigner
“Pop Style” – Drake Featuring The Throne
“All The Way Up” – Fat Joe & Remy Ma Featuring French Montana & Infared
“That Part” – ScHoolboy Q Featuring Kanye West

BEST RAP/SUNG COLLABORATION
“Freedom” – Beyoncé Featuring Kendrick Lamar
“Hotline Bling” – Drake
“Broccoli” – D.R.A.M. Featuring Lil Yachty
“Ultralight Beam” – Kanye West Featuring Chance The Rapper, Kelly Price, Kirk Franklin & The-Dream
“Famous” – Kanye West Featuring Rihanna

BEST RAP SONG
“All The Way Up” – Fat Joe & Remy Ma Featuring French Montana & Infared
“Famous” – Kanye West Featuring Rihanna
“Hotline Bling” – Drake
“No Problem” – Chance The Rapper Featuring Lil Wayne & 2 Chainz
“Ultralight Beam” – Kanye West Featuring Chance The Rapper, Kelly Price, Kirk Franklin & The-Dream

BEST RAP ALBUM
Coloring Book – Chance The Rapper
And The Anonymous Nobody – De La Soul
Major Key – DJ Khaled
Views – Drake
Blank Face LP – ScHoolboy Q
The Life Of Pablo – Kanye West

BEST COMPILATION SOUNDTRACK FOR VISUAL MEDIA
Amy – Various Artists
Miles Ahead – Miles Davis & Various Artists
Straight Outta Compton – Various Artists
Suicide Squad (Collector’s Edition) – Various Artists
Vinyl: The Essentials Season 1 – Various Artists

BEST SONG WRITTEN FOR VISUAL MEDIA
“Can’t Stop The Feeling!” – Justin Timberlake, Anna Kendrick, Gwen Stefani, James Corden, Zooey Deschanel, Walt Dohrn, Ron Funches, Caroline Hjelt, Aino Jawo, Christopher Mintz-Plasse & Kunal Nayyar
“Heathens” – Twenty One Pilots
“Just Like Fire – “P!nk
“Purple Lamborghini” – Skrillex & Rick Ross
“Try Everything” – Shakira
“The Veil” – Peter Gabriel

PRODUCER OF THE YEAR, NON-CLASSICAL
Benny Blanco
Greg Kurstin
Max Martin
Nineteen85
Ricky Reed

BEST MUSIC VIDEO
“Formation” – Beyoncé
“River” – Leon Bridges
“Up & Up” – Coldplay
“Gosh” – Jamie XX
“Upside Down & Inside Out” – OK Go

Categories
E! News

Chibby K Solja ndio mfalme wa Run The Beat Freestyle Battle

Mshiriki Chibby K Solja Jumapili usiku aliibuka mshindi wa jumla wa mitindo huru ‘FreeStyle’ katika mpambano mkali na wa kuvutia uliokuwa ukiendeshwa na kipindi cha Run the Beat cha Coconut FM kinachoitwa Run the beat Free Style Battle 2017.

Shindano hilo ambalo lilifikia tamati baada ya jumla ya wasanii wa mitindo huru 5 kuchuana vikali ili kumpata mshindi wa jumla kwa mwaka 2017 ambapo shindano hilo lilianzia katika hatua ya robo fainali.

Majaji wa shindano hilo ambao walikuwa pamoja aliyekuwa mshindi wa Freestyle Zanzibar mwaka 2012 Chabby Six na mmoja wa rapa kutoka kundi la Zee Town Sojaz, kira Kirami ambapo walimtangaza Chibby K kama mshindi wa shindano ya mitindo huru.

Chibby K (aliyevaa flana nyekundu) akikumbatiana na mpinzani wake Devil baada ya kutangazwa mshindi katika mashindano ya Run The Beat Freestyle Battle

Aidha katika fainali hizo kazi haikuwa ngumu kuamua mshindi ilipofika fainali kwani Chibby K alifanya kile ambacho mashabiki hawakukitarajia kwa kumwaga mashairi makali dhidi ya mpinzani wake Devil ambaye hakuweza kujibu mapigo hayo vizuri na kuonekana dhahiri kuwa taji limeenda kwake, ambapo hata mashabiki walikuwa wanamkubali ile mbaya.

Katika fainali hizo za Freestyle zilizofanyika katika Club ya usiku ya Intebe iliyopo maeneo ya Chukwani, wasanii na makundi ya Breakdance yalitoa burudani katika mashindano hayo.

Mshindi wa Run the Beat Free Style, Chibby K alijishindia mkataba wa kurekodi nyimbo moja audio kutoka studio za Mandevu records na video kwa director Huruma pamoja na promosheni, pia mshindi wa pili, rapa Devil amepata ofa ya kurekodi wimbo mmoja kutoka producer Bonge Jr.

Categories
E! News

Video: Trailer ya 2 ya filamu mpya ya maisha ya Tupac kuachiwa siku yake ya kuzaliwa June 16

Kwa muda mrefu mashabiki walikuwa na hamu ya kuiona filamu inayoonyesha maisha ya rapa wa Marekani hayati Tupac Shakur inayoitwa ‘All Eyez On Me’ inatarajiwa kuachiwa kwenye sinema katika siku yake ya kuzaliwa June 16.

Katika filamu hiyo waigizaji kama Danai Gurira amechukua uhusika wa marehemu mama yake Tupac, Afeni Shakur, Demetrius Shipp Jr. kama Tupac, Jamal Woolard akiwa kama Notorious B.I.G. na Dominic L. Santana akiwa kama Suge Knight.

Filamu hiyo imetengenezwa na kampuni ya Lionsgate na kuongozwa na Director Benny Boom.

Angalia trailer hiyo hapo chini.