Categories
E! News

Producer Buju Mandevu afiwa na mama yake mzazi

Mama Mzazi wa mtayarishaji wa muziki kutokea visiwani Zanzibar, Abubakar almaarufu kama Buju Mandevu amefariki dunia leo Jumamosi Oktoba 12, 2019 akiwa nyumbani kwake maeneo Majestic ndani ya Mji Mkongwe.

Taarifa ya kifo hicho, imethibitishwa na familia ya producer na mipango ya mazishi yanatayarishwa na familia na taarifa itatolewa. Zenji255 inatoa pole kwa familia ya Buju Mandevu kwa msiba mzito alioupata na mungu atamfanyia wepesi katika kipindi hiki kigumu.

Endelea kufuatilia Zenji255 katika mitandao yetu kwa taarifa zaidi.

Categories
E! News

Picha: Producer wa Mandevu Records, Buju afunga ndoa

Producer wa Mandevu Records, Buju ameisaliti kambi ya mabachelor mastaa wa visiwani Zanzibar kwa kufunga ndoa jana Ijumaa Oktoba 29.

Zenji255 inawapongeza Producer buju na mkewe kwa kufunga ndoa na tunawatakia safari ya maisha ya pamoja yenye furaha tele.

Angalia picha za harusi hapo chini

14 18 30 27 34 4 7 13 11 8