Categories
Videos

New Video: Alatish Mabawa ft. Chillah – Dede

Alatish Mabawa anawakaribisha kuangalia video ya wimbo wake mpya unaitwa “Dede” akiwa amemshirikisha Chillah. Video imetayarishwa na Kwetu studio.

Angalia video hiyo na utoe maoni yako.

Categories
Videos

New Video: Alatish Mabawa – Bora mimi

Kama tayari umeshausikiliza wimbo mpya wa msanii wa muziki Alatish Mabawa, na kama bado bonyeza hapa kwa kuusikiliza. Baada ya kuupata wimbo huo na Alatish Mabawa anaweletea video ya wimbo huo mpya unaitwa “Bora Mimi”. Video imetayarishwa na director Kenny.

Angalia video hiyo na utoe maoni yako.

 

Categories
Music

New Music: Alatish Mabawa – Bora Mimi

Msanii wa muziki kutokea visiwani Zanzibar Alatish Mabawa ameachia wimbo mpya unaitwa “Bora Mimi”. Wimbo umetayarishwa na producer Lil Ghetto na Flavor Noma.

Sikiliza wimbo huo na utoe maoni yako.

 

Categories
Videos

New Video: Alatish Mabawa – Barua

Msanii wa muziki Alatish Mabawa ameachia video ya wimbo wake mpya unaitwa “Barua”. Kama bado hujaupata wimbo wake bonyeza hapa. Video imetayarishwa na Director Anko Jo.

Angalia hapo chini na utoe maoni yako

Categories
Music

New Music: Alatish Mabawa – Barua

Huu hapa mwingine ni wimbo mpya kutoka kwa Alatish Mabawa unaitwa ‘Barua’. Wimbo umetayarishwa katika studio za Akhenaton Records na producer Lil Ghetto.

Sikiliza hapo chini na utoe maoni yako.

 

Categories
Videos

New Video: Alatish Mabawa – Machozi

Msanii Alatish Mabawa ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Machozi’. Video imetayarishwa na Director Lucky.

 

Categories
E! News

Video Teaser: Mabawa kuachia video ya ‘Machozi’ Oktoba 28

Msanii wa muziki Alatish Mabawa ambae hivi karibuni aliachia wimbo wake mpya wa Machozi uliotayarishwa katika studio za Akhenaton Records, hivi karibuni ametoa ahadi kuachia video ya wimbo huo Oktoba 28.

mabawa

Akiongea na Zenji255 Mabawa amesema kuwa Video ipo katika matayarisho ya mwisho ambayo imesimamiwa na Director Unlucky, na anatarajia kuachia Jumamosi ya wiki hii tarehe 28 katika vituo vyote vya TV nchini.

“Video tumefanya katika maeneo tofauti ikiwemo Nungwi katika hoteli ya ZALU ambapo mpaka kumaliza video nzima imenigharimu kama milioni 4 ambayo nililipia baadhi ya maeneo gharama za chakula pamoja na director kumlipia gharama zake za matengenezo ya video. Ila nashukuru mungu kila kitu kimeenda sawa” Amesema Mabawa.

Angalia kipande kifupi cha video hiyo.

 

Categories
Music

New Music: Machozi – Mabawa

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutokea Zanzibar, Alatish Mabawa ameachia wimbo wake mpya unaoitwa “Machozi”. Wimbo umetayarishwa katika studio za Akenaton Records chini ya producer Lil Ghetto.

Sikiliza hapa na utoe maoni yako

 

Categories
E! News

Alatish Mabawa kumtambulisha ‘Twarity’ na wimbo wake mpya Jumatatu ijayo

Msanii wa muziki Alatish Mabawa kupitia lebo yake ya ‘Mabawa Classic’ Feb 20 atamtambulisha rasmi msanii mpya ‘Twarity’ ambaye tayari ameshatengeneza wimbo mpya unaoitwa ‘Kipenda Roho’ ambao ameshirikishwa Mabawa.

alatish mabawa

Akiongea na Zenji255, Mabawa amesema kuwa hadi sasa tayari ameshasaini msanii mmoja na bado na mipango ya kuwasaini wengine ambao watakuja kutangazwa siku za mbele.

Kwa upande wake amesema kuwa amechukua uamuzi huo baada ya kuona vipaji Zanzibar vinaibuka vipya kila siku.

“Zanzibar vipaji vipo vingi tu ila msaada wa kuvinyanyua ni mdogokuna wasanii wazuri mtaani. Nimeamua kuanzisha lebo ili kuwasaidia wasanii wenye vipaji kuonyesha uwezo wao, kupitia lebo yangu nataka kuleta mapinduzi. Na bado nina mipango mingine tofauti na muziki katika kuendeleza vipaji vipya vya hapa Zanzibar” Amesema Mabawa

Wimbo wa msanii Twarity umetengenezwa katika studio za Six Records na producer Side to The Lee akiwa pamoja na Chilly K.

Categories
E! News

Exclusive: Wari wengi wa sasa ndoa zao hazidumu muda mrefu – Alatish Mabawa

Msanii Alatish Mabawa baada ya kuachia wimbo wake mpya ‘Wari wa leo’ aliomshirikisha Khadija Kopa azungumzia sababu ya kuupa jina la wimbo huo ni kutokana na wari wengi ndoa zao zinaharibika mapema pasipo na watu wanavyotegemea.

mabawaKatika mahojiano aliyofanya na kipindi cha Run the Beat , Mabawa anasema kuwa aliamua kuupa wimbo huo wari wa leo kwa sababu ukiangalia wanawake wengi wana matatizo mengi katika ndoa zao kuliko wanaume.

“Katika kuzungumzia wari wa leo niliona ni vizuri kumtafuta mwari wa zamani (Khadija Kopa) awemo katika wimbo wangu halafu na mimi nikachukua uhusika wa kuwazungumzia wari wa sasa na jinsi wanavyotakiwa waishi kama wari wa zamani” Alifafanua Mabawa.

Sikiliza Exclusive Interview hiyo hapa chini.

Categories
Music

New Music: Alatish Mabawa ft Khadija Kopa – Wari wa Leo

Msanii Alatish Mabawa baada ya kufanya vizuri na wimbo wa ‘Leo Kesho’ na sasa anatambulisha wimbo wake mpya ‘Wari wa Leo’ akiwa amemshirikisha malkia wa mipasho ‘Khadija Kopa’. Wimbo umeteyarishwa na producer Lil Gheto katika studio za Akhenaton.

Sikiliza hapa na utoe maoni yako.

Categories
E! News

Alatish Mabawa kuja na ‘wari wa leo’ na kuzindua albamu mpya hivi karibuni

Msanii Alatish Mabawa baada ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa wiki kadhaa zilizopita, Alatish ameamua kutoa zawadi ya ‘Birthday’ kwa mashabiki wake ambapo ataachia wimbo wake mpya ‘Wari wa Leo’ siku za hivi kaaribuni kuanzia sasa.

alatish mabawa

Akizungumza na Zenji255 Mabawa alisema kuwa anamshukuru mungu mpaka hapo alipofika na anatarajia kuja na zawadi kubwa kwa mashabiki wake kwani hivi karibuni ataachia wimbo mpya na utafuata uzinduzi wa albamu yake mpya baada ya kuachia wimbo huo.

“Katikati ya wiki hii tukijaaliwa natarajia kuachia kazi yangu ya mwisho ambayo itakayofunga albamu yangu ninayotaka kuizindua. Na wimbo unaitwa Wari wa leo, nimemshirikisha malkia wa mipasho Khadija Kopa na wimbo nimefanya katika studio za Akhenaton.” Alatish Mabawa alielezea.

Categories
E! News

‘Fiesta ndio show yangu ya kwanza niliyolipwa hela haijawahi tokea’ – Alatish Mabawa

Hit maker wa wimbo mpya ‘Leo Kesho’ kutokea Zanzibar, Alatish Mabawa amefunguka kuhusiana jambo analokumbuka akiwa katika tasnia ya muziki kwa mara ya kwanza ni baada ya kuuachia wimbo wake wa kwanza uliomtabulisha.

mabawaAkizungumza na Zenji255 Mabawa alisema kuwa Tamasha la Fiesta ndio ilikuwa show yake ya kwanza kushiriki na alilipwa pesa ambayo haijawahi kuvunja rekodi ya kulipwa pesa nyingi hadi hivi sasa.

“Ilikuwa ni 2010 Fiesta ilifanyika Zanzibar,  na nahisi yote yalitokana na mashabiki walipenda wimbo niliokuwa naimba lakini mimi mwenyewe nikiisikiliza najiuliza huu wimbo wameupendea nini, yaani mimi mwenyewe mpaka nacheka.” Mabawa aliongezea

 

Categories
Music

New Music: Alatish Mabawa – Leo Kesho

Wimbo mpya kutoka kwa msanii wa kizazi kipya Alatish Mabawa unaitwa ‘Leo Kesho’. Wimbo umetayarishwa katika studio za Akhenaton records chini ya producer Lil Ghetto.

 

Categories
E! News

Alatish Mabawa kuachia wimbo mpya ‘Leo Kesho’ Jumatatu hii

Msanii wa kizazi kipya Zanzibar Alatish Mabawa anatarajia kuachia wimbo wake mpya wa ‘Leo Kesho’ Jumatatu hii.

mabawaAkizungumza na Zenji255 Mabawa alielezea kuhusu ukimya wake wa muda mrefu ni kutokana na kuachia kazi mara kwa mara lakini mafanikio yalikuwa hayaonekani ndipo akaamua akae chini na kujipanga upya.

Mabawa aliongezea kuwa “Leo Kesho ni wimbo wangu mpya natarajia kuuachia Jumatatu ya wiki inayokuja (22, Agosti) na huu ni wimbo ambao wa kikubwa sana. Kwani ukiusikiliza wimbo huo utaona tofauti ya kiuandishi, uimbaji na kama itasapotiwa kwa nguvu zote basi inaweza ikapeperusha bendera ya Zanzibar.”

Categories
E! News

Nasikitika nafanya kazi kubwa lakini ‘Support’ inakuwa ndogo – Alatish Mabawa

Na Mkali Nesta

Mkali wa tungo tamu anaetokea Zanzibar, Alatish Mabawa  amefunguka yanayohusu katika muziki wake ya kuwa ‘support’ kwa upand wake kimuziki bado ni ndogo na inampa wakati mgumu kwa yeye mwenyewe. Akizungumza na Zenji255 alisema kuwa “kiukweli najitahidi kukaza buti lakini nahisi kuna mtu analegeza nyuzi za viatu vyangu. Unajua mimi sina ugomvi na wala sina beef na mtu nasikitika nafanya kazi kubwa lakini support inakua ndogo baadhi ya sehemu sijui kitu gani labda ‘some time’ binadamu anazaliwa hivyo anakua na nyota mbaya kwa watu lakini kinachonipa moyo nikwamba raia bado wanaimani kubwa na mimi kutokana na huduma ninazozitoa wanazielewa ndio maana sikati tamaa” Kuhusiana na wimbo wake mpya uitwao Woro woro, Mabawa amesema ijumaa hii anatarajia kuachia wimbo huo ukiambatana na uzinduzi wa video ya nyimbo hiyo Kwa upande mwingine alatish aliwataka watangazaji pamoja na maDj kuzitangaza kazi za nyumbani na kuwafanya mashabiki wawe na imani na mziki wao.