Taarifa rasmi kwa wasomaji wetu wa zenji255.com

0

Habari zenu mabibi na mabwana? Kwanza, tunapenda kumshukuru mungu muweza wa kila kitu kwa kuweza kujaalia mtandao huu wa zenji255.com kurudi katikia hali yake ya kawaida. Pili, tunapenda kuwashukuru wale wote waliofanikisha mtandao wako wa zenji255.com kuweza kurudi hewani baada ya kupata hitilafu siku za hivi karibuni.

Mnamo Machi 8, 2017 siku ya Jumatano majira ya saa tatu na dakika ishirini asubuhi, zenji255 Media kupitia blog yao ya Zenji255.com ilidukuliwa (Hacked) na watu wasiojulikana. Ambapo udukuzi huo ulisababisha zenji255.com kupoteza ma-file mengi ya habari na matokeo yake watu hao waliofanya udukuzi kufuta ma-file hayo na kuweka ya kwao.

Haijajulikana mpaka sasa chanzo kilikuwa ni nini mpaka watu hao wakaamua kufanya hivyo na tumejaribu kufuatilia katika vyombo vyote sheria na kuripoti, ila tunashukuru kwa kufanikiwa kuweza kupata data zote.

Tunaomba radhi kwa tatizo lolote litakalojitokeza endapo utakuwa umekwazika wakati ukitafuta habari ambayo katika mitandao yetu ya kijamii ipo lakini kwenye blog hakuna, kwani katika blog ya zenji255.com habari ya mwisho ilitoka tarehe Machi 7, 2017 lakini tumefanikiwa kurudisha data kuanzia Machi 3, 2017.

Uongozi wa zenji255 Media Group unapenda kutoa shukuran za dhati kwenu na nasi bega kwa bega na tunapenda kuwatakia kuwatakia siku njema na mungu awabariki.

Ahsanteni

Razakey Tausir (Mkurugenzi Mtendaji)