I.T kuandaa Bonanza maalum kwa ajili ya kuwasaidia watoto yatima na wazee

0

Msanii I.T kwa mara ya kwanza ameandaa bonanza ambalo kalipa jina la ‘Uzalendo’ kwa ajili ya kuwasaidia watoto yatima na wazee ambalo litafanyika katika uwanja wa Aman Zanzibar.

Akiongea na Zenji255 I.T amesema kuwa bonanza hilo litakuwa likichangisha fedha kwa ajili ya watoto yatima waliokuwepo katika vya kulelea watoto hao na kuwasaidia wazee waliokuepo katika nyumba za wazee Seblen.

“Mimi ni binadamu na huwa ninaguswa sana na ndugu zangu waliopoteza wazee wao maisha ambayo wanayoishi sio kama wengine kwani huwa wana mawazo mengi akimuona mwenzake ana wazee wote wawili. Vile vile nimeamua kuwasaidia wazee wetu waliokuwepo katika vituo vya wazee, Amani.” Alisema I.T

Katika bonanza hiyo litapambwa na mechi ya mpira wa miguu kati ya Charawe FC na Gulioni City na litasindikizwa na wasanii mbali mbali kutokea Zanzibar akiwemo Jumaa Town, Sister Rahima, Mabawa, Alfa, Jobfire, Hemedy Music, Buyubaya Mtabiri, Tarik Shadeed na Waiz Boy.

Bonanza hilo litafanyika tarehe 25 Disemba katika uwanja wa Amani Zanzibar saa 2:00 Usiku.