I.T atangaza rasmi kujivua uanachama wa Chama cha wasanii Zanzibar (Z.F.U)

1

Msanii mkongwe wa muziki wa Zenji Fleva,Iddi Thabit (I.T) ambaye pia alikuwa kiongozi wa nidhamu katika chama hicho, Jumapili hii ametangaza rasmi kujivua uanachama wa chama cha wasanii wa muziki kipya Zanzibar.

umejivuruga

Akiongea na Zenji255 I.T alisma kuwa tatizo lililokuwepo katika chama hicho cha wasanii hakiangalii wasanii wapya ambapo pale kazi za serikali au binafsi zinapotokea na wala hawashirikishwi wasanii wote bali ni kupeana wenyewe kwa wenyewe.

“Ni kweli nimetangaza rasmi kujivua uanachama wa Z.F.U kutokana na ubaguzi unaoendelea ndani ya chama hicho kikubwa zaidi kinachonishangaza kuona kila siku nyimbo au kazi za serikali zinaimbwa na wasanii wale wale hawataki kuwapa wasanii wengine nafasi ya kuonesha vipaji vyao.” Amesema I.T.

Aliongezea kuwa ” Kwasababu kuna wasanii wengi wachanga wamekuja sasa hivi kwenye game na wanafanya vizuri kwanini wasipewe nafasi wakaonesha uwezo wao? Kwa hivi sasa tunajipanga kuanzisha chama chetu na waanzilishi tutakuwa mimi, Buju, Mabawa na Rama B, ili kuleta maendeleo katika mziki wa Zanzibar.” Alimalizia I.T