Sultan King, Chidy Grenade watembelea studio za Wasafi

0

Wasanii wa muziki kutokea visiwani Zanzibar, Sultan King na Chidy Grenade hivi karibuni wameonekana wakiwa picha ya pamoja na Diamond Platnumz katika studio za Wasafi (WCB).

Sultan king
Sultan King (Kushoto), Diamond Platnumz (Katikati) na Chidy Grenade (Kulia) wakiwa katika picha ya pamoja ndani ofisi za WCB

Akiongea na Zenji255 Sultan King amesema kuwa ilikuwa ni kama siku nzuri kwao kutembelea ofisi ya WCB kwani waliona mambo tofauti na kazi mbali mbali zinazohusiana na muziki zikitendeka WCB.

“Kikubwa kwanza nitumie nafasi hii kumpongeza Diamond kwa kuwa na mawazo mapana zaidi.kwa sababu kiukweli kwa wasanii wengi wa Tanzania na Waafrika wengi tunaweza tukawa na kipaji lakini mazingira yetu ya kazi yanakuwa magumu.” Amesema Sultan King.

Na kwa upande Chidy Grenade amesema kuwa “Nimefurahi kuona maendeleo ya mwanamuziki mwenzangu na kila jambo lina wakati wake, kwa sasa siwezi sema tumekubaliana na ndugu yetu ila watu wetu wakae mkao wa kula kutoka kwa uongozi wa Tausi” Amemalizia Chidy.