Stone Town Records kufanya Cypher ya Hip Hop, Novemba 4

0

Lebo ya muziki kutokea visiwani Zanzibar, Stone Town Records imeandaa kilinge cha Hip Hop ambacho kitakuwa kinasaidia watu mbali mbali kuelewa mambo tofauti yanayohusu muziki wa Hip hop.

stone town

Akiongea na Zenji255 mmoja wa waanzilishi wa kilinge hicho Mash Marley amesema, lengo kubwa ni kuwasaidia wasanii wa muziki tofauti kujua baadhi ya sheria na historia za muziki wa Hip Hop tangu kuanza kwake mpaka sasa ulipo.

“Tumeamua kuanzisha Cypher kwa upande wa Zanzibar kuwasaidia pia wasanii wanaochipukia ambao wanafanya muziki wa Hip Hop. Ukiangalia Zanzibar wanaofanya Hip Hop sio wengi na kuna vipaji mitaani vimejificha na sisi hatujui nadhani hii ndio sehemu ambayo wao wanaweza wakajulikana” Amesema Mash.

Kwa upande huo huo Mash ameongezea kuwa katika kilinge hicho shuhuli zitakazokuwepo ni kama kujua historia, sheria na misingi ya Hip Hop vile vile kubadilishana mawazo na wasanii kutoka nchi mbali mbali pamoja na kufanya mitindo huru (Freestyle).