Stone Town Records kuandaa na warsha kwa ajili ya watayarishaji wa muziki Zanzibar, Novemba 9

0

Lebo ya muziki ya Stone Town Records iliyopo maeneo ya Mji Mkongwe imeandaa warsha kwa watayarishaji wa muziki visiwani Zanzibar ambayo itakuwa ikifundisha mambo mbali mbali ikiwemo jinsi ya kutayarisha na kutengeneza muziki (Mixing and Mastering).

stone town recordsMmoja wa waandaji na mkurugenzi wa mipango katika lebo hiyo, Mash Marley amesema kuwa madhumuni ya warsha hiyo ni kuweza kusaidia watayarishaji chipukizi na wakongwe ambao wapo katika soko la muziki hapa Zanzibar.

“Kuna methali inasema, Elimu haina mwisho. Na lengo letu ni kuifikisha hii elimu kwa watayarishaji wetu ambao wanafanya kazi hapa kwetu. Tunataka muziki wetu uwe mzuri na wenye ubora wa hali ya juu, Zanzibar ina vipaji vizuri katika kutayarisha muziki tatizo elimu kama hizi zinakuwa ngumu kupatikana hapa kwetu” Amesema Mash Marley.

Warsha inatarajiwa kuanza siku ya Alhamis Novemba 9 itakayoanza saa nane mchana mpaka saa kumi na moja jioni, katika ukumbi wa studio ya muziki na filamu iliyopo Rahaleo, ambapo mkufunzi wa warsha hiyo atakuwa DJ Contours kutoka Ujerumani.