Steve RnB amtaka Nuruelly atafute mshauri katika muziki wake

0

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Steve RnB amefunguka na kusema kuwa katika wasanii wa kuimba Tanzania msanii Nuruelly anakipaji kikubwa sana na ana uwezo wa hali ya juu kiasi kwamba anaweza kufanya mambo makubwa kwenye muziki wa bongo fleva.

steve rnb

Steve RnB alisema hayo kupitia kipindi cha eNewz na kusema kuwa Nuruelly anastahili kupata washauri wazuri ambao wanaweza kumshauri vyema kuhusu muziki wake na akafanya jambo kubwa katika muziki kutokana na kipaji chake.

“Nulipokuwa Uturuki nilikuwa nawasiliana na Nuruelly nilikuwa sijajua kama ametoa ngoma ya ‘singeli’ kiukweli kabisa kati ya wasanii ambao wapo talented basi ni Nuruelly, ni mtu ambaye ana sauti nzuri ambayo siku zote mimi sijawahi kusikia sehemu nyingine, hivyo ni mtu ambaye anaweza kufanya kitu kikubwa zaidi ya hicho alichofikiria ni kiasi tu cha kukaa chini na kujua kitu gani anataka na anaweza kufanya kitu kizuri zaidi, yaani akutane tu na watu wazuri ambao wanafikiria vitu vizuri zaidi wamshauri vizuri, naamini yeye mwenyewe ataona ni kitu gani anatakiwa kukifanya” alisema Steve RnB