Smile na Sultan King kulimaliza bifu lao kwenye ‘Toriro’ Jumatatu hii

0

Heshima ya muziki wa zanzibar unazidi kupewa nguvu baada ya wasanii wawili kusemekana walikuwa hawakai zizi moja kutokana na uhasama waliokuwa nao watu hao wawili.

Lakini hivi karibuni Smile alionekana kuandika taarifa ambayo ya kushangaza katika ukurasa wake wa Facebook baada ya kuweka cover ya wimbo wake mpya ambao unatarajiwa kuachiwa Jumatatu hii ya Juni 8 na kuonekana ya kuwa ilikuwa ni KIKI ya wimbo mpya.

Wimbo huo unaitwa ‘Toriro’ ambapo Smile amemshirikisha Sultan King na wimbo umetayarishwa na Producer Bonge JR.