Smile na I.T waamua kuzungumza kuhusiana na ugomvi uliokuwepo kati yao

0

Kwa mbio za wasanii wa Zanzibar na mwendo wanaoenda nao hivi sasa muziki wa Zanzibar unaweza ukaelekea pahala sio pazuri.

ugomvi

Ugomvi kati ya msanii na msanii kiupande mwingine haiwezi kusaidia muziki wa jamii fulani kukaa katika sehemu nzuri na yenye kuleta manufaa japokuwa wengine husema itaweza kumpa umaarufu msanii kwani kila wakati atakuwa anatajwa jina lake kutokana tukio husika lililomkuta.

Nadhani kwa Zanzibar ni muda mrefu wasanii wa Zanzibar wanajitahidi kila siku kuliweka soko lao la muziki Zanzibar likae katika (level) muelekeo mzuri lakini inashindikana kutokana na chuki, ubinafsi pamoja na kutokuwa na umoja. Na ni nini kinasababisha haya?

Zenji255  ilikaa chini na kuongea na wasanii wa muziki wa kizazi kipya I.T na Smile kwa nyakati tofauti ambapo hivi karibuni walionekana kutoelewana huku wakirushiana maneno kupitia mitandao ya kijamii.

I.TMsanii I.T alisema kuwa kwa upande wake hajawahi kugombana na mtu yoyote kwani huenda ikachangia muziki na maisha yake yakakaa sehemu mbaya kwani ugomvi huenda ukasababisha chuki.

“Mimi ninachoshangaa Smile nikikutana nae naona haniambii lolote kama kuna kitu nimemkwaza ama la, naona tunasalimiana vizuri. Kwanza, Smile anatakiwa afahamu kwamba mimi ni mkongwe wa muziki na mimi siwezi kushindana na watoto wadogo kama yeye anatafuta ‘kiki’ kwa sababu ya wimbo wake una mapungufu kwahiyo akitumia jina langu anaweza akaupatia umaarufu, muziki hauendi kinamna hiyo” Amesema I.T

I.T Alimalizia kiupande kuwa “Ninachomshauri Smile afanye kazi na aandike mashairi mazuri basi atafanya vizuri asiwe na wivu na mafanikio yangu kama ndio kinachomuumiza.”

smile

Na Smile nae amesema kuwa alishawahi onana na I.T na hakuona dalili yoyote na kwake yeye anamuheshimu kutokana I.T kuwepo katika muziki katika kipindi kirefu.

Amesema¬† Smile “Mimi kwa sasa siwezi nikafikiria kugombana kuhusiana na wasanii wa Zanzibar kwa sababu kila mtu anafanya muziki wake. I.T namfahamu ni mkongwe hapa Zanzibar na vile vile mimi na yeye, yeye yupo kwa kipindi kirefu na anafahamu mambo mengi kuhusiana na muziki wetu lakini kwanini aniongelee mimi mtoto mdogo niliyeanza juzi.”

“Nimekaa mwaka mzima sijaaachia hata wimbo mmoja lakini baada kuachia ‘Saa Ngapi’ nimeanza kuongelewa kwa ubaya. Mimi siwezi nikatafuta kiki kupitia kwake yeye kuna wasanii kibao ninawafikiria kama Diamond, Ali Kiba na Rayvanny, ambao wana mafanikio makubwa katika muziki na yananiumiza¬† kichwa kila siku ili kuwa kama wao ni sio kama I.T” Ameongea Smile.