Sister Rahima awalalamikia wasanii wa Zanzibar wanaokatisha tamaa wenzao

0

Msanii wa mziki wa kizazi kipya mwanadada Rahima amelalamika kuhusiana na tabia ya  wasanii wa Zanzibar ya kuwakatisha tamaa wasanii wenzao pale wanapoomba msaada kwenye muziki.

rahimaAkiongea na Zenji255 Rahima amesema kuwa alishawahi kuomba msaada wa kufahamishwa mambo mbali mbali yanayohusu muziki yeye akiwa kama msanii apate kuyafahamu lakini matokeo hakuambulia chochote zaidi ya maneno machafu.

“Kuna baadhi ya wasanii kiukweli wanajiona wao ndio kila kitu sikupendezewa kabisa na kitendo kile. Msanii nilimuomba vizuri na kwa heshima tu lakini alinitukana na kunidharau wakati yeye mwenyewe bado hajafika popote.” Amesema Rahima.