Sina uhusiano wowote na I.T ila nililipenda sana wazo la ‘Ushanivuruga’ na mimi nikatoa ‘Umejivuruga’ – Faay Baby

0

Baada ya msanii I.T kutoka malalamiko ya ‘remix’ ya wimbo wa ‘Umejivuruga’ uliofanywa na Faay Baby, mwanadada huyo ameamua na yeye kusema kuwa hakuna uhusiano wowote kati ya wawili hao.

faay baby

Akizungumza na Zenji255 Faay Baby anasema kuwa yeye anajua kama kuna wimbo unaitwa Ushanivuruga na alikuwa anapenda kila siku kuusikiliza wimbo huo na ndio maana akaamua kufanya remix yake kama kumjibu I.T.

“Siku ya kwanza tu Ushanivuruga inatambulishwa kwenye redio, niliipenda sana idea ya wimbo ule na nikaamua kulichukua hilo wazo na kuligeuza kinyume yake yaani kama namjibu I.T kutokana na wimbo wake unavyosema.” Faay Baby alielezea.