Siku ya 5: Angalia picha za matukio mbalimbali katika Tamasha la ZIFF

0

Ikiwa zimesalia siku kadhaa kuendea mwishoni mwa tamasha la filamu za nchi za majahazi (ZIFF), kwa siku ya jana (Jumatano, Julai 12) wananchi wengi walihudhuria katika tamasha hilo ambapo walianza kuangalia filamu na baadae kuhamia kwenye upande wa burudani.

Mohammed Issa Matona ndie ambae aliyetoa burudani kwa usiku wa jana na kikundi chake cha G Clef band ambapo kilisindikizwa na wanamuziki maarufu mbali mbali kutoka Tanzania kama vile Makame Faki, Mohammed Ilyas, Spider Bashan na wengine wengi.

Angalia picha hapo chini ujionee.