“Sikatai kufananishwa na msanii yoyote kikazi ila…” – Chaby Six

0

Rapa kutokea visiwani Zanzibar Chaby Six ametoa malalamiko yake juu ya watangazaji wa maredio na TV visiwani Zanzibar kuhusiana na kusema maneno yasiyo ya kweli juu yake.

chaby six

Chaby Six ameambia Zenji255 kuwa alitoa malalamiko hayo baada ya kusikia katika redio moja hapa visiwani ikisema kuwa yeye anatafuta kiki ya kutengeneza beef na wasanii kwa makusudi.

Mimi moyo wangu msafi na kama ndio kiki sihitaji kiki wala snea sina mgongo wa kumtoa mtu kwa njia hii… sina beef na mtu maana ni uhasama na mimi sitaki uhasama na mtu. Bora jigambeeee, nipondeee ila usitangaze kuwa beef na mimi.” Amesema Chaby Six.

Ameongezea kuwa “Kila mtu atoke kivyake, tusiharibiane CV tulizo nazo sasa, Chaby fujo ameacha zamaaani, sasa mimi ni good boy.”