‘Sijabahatika kuoa bado ila natangaza ndoa kama kuna mchumba anaetaka kuolewa’ – Mantuzzo

0

Msanii wa kizazi kipya kutoka Zanzibar, Mantuzzo amefunguka kuhusiana na taarifa zinazoenea mitaani kwa kuambiwa kuwa ameoa kimya kimya.

mantuzzoAkizungumza na Zenji255 Mantuzzo “Kiukweli kwa kuoa bado sijaoa ila hizo tetesi nazisikia na mimi kwa sasa nathibitisha kuwa sio za kweli na mimi bado sijaoa.”

“Lakini kama mchumba anaetaka nimuoe hakuna tatizo awe mwenye heshima, mwenye upendo na awe ni mtu ambae anajali na anajua nini maana ya ndoa ni moja hatua ya mwanadamu hiyo ” Aliongezea Mantuzzo.