‘Sihusiki katika kuvujisha wimbo wa Abramy aulizwe vizuri’ – Chilly K

0
Baada ya msanii Abramy kulalamika kuwa Producer wa Action Music kuvujisha wimbo wake mpya ‘Nashindwa’ ambao alitegemea kuuachia mwezi huu Novemba 20.
chilly k
Lakini katika kila malalamiko, ni vyema kusikiliza pande zote zinazohusika kwenye jambo husika ili kuupata ukweli. Action Music ndio walioutayarisha wimbo huo wamezungumza kuelezea mambo yalikuwaje.
Producer wa studio hiyo, Chilly K ameiambia Zenji255 kuwa yeye hana taarifa yoyote ya wimbo huo kuuvujisha, kwani siku iliyorekodiwa wimbo huo walikuwepo wawili tu na hakuna alieondoka na wimbo.
“Ngoma  ipo tayari na ilikuwa katika masahihisho madogo madogo ya kumaliziwa ili iende redio, lakini mimi sihusiki katika kuvujisha. Uongozi wangu hauniruhusu mimi kupeleka nyimbo za wasanii redio. Kuna watu maalum wanahusika katika upelekaji redio, Itabidi aulizwe vizuri (Abramy) kuhusiana na hili mwenyewe itakuwa anamuelewa mhusika aliyefanya hivyo” amesema Chilly K.