Side to the Lee atangaza kufunga ndoa Mei 27

0
side

Producer na mmiliki wa studio ya Six Records, Side to the Lee. Ametangaza kuvuta jiko na kuiaga kambi ya mabachela rasmi mnamo Mei 27, baada ya kukaa katika uhusiano wa muda mrefu na mchumba wake.

Akizungumza katika kituo cha redio, Side to the lee alifunguka na kusema kitu ambacho kilichomshawishi mpaka akaamua kufunga ndoa na akasema kuwa ameamua kuepuka na matamanio. “Kiukweli kuna vitu vingi sana vimenifanya kufanya maamuzi hayo kwa sababu sisi ni binaadamu na ukiangalia upande mwingine dini yetu ilivyo, mtu ukibalehe unatakiwa upatiwe mke kwa sababu tunakula na kushiba.” Alisema Side.

Kwa upande mwingine Side alizungumzia kuhusiana na kuacha muziki wakati akiwa katika maisha ya ndoa, alisema “Kwanza muziki bado naudai, kwahiyo ikifika muda nitasema basi, na kila mtu ana maisha yake na malengo baada ya muda flani nataka niweje, na ni kweli nina mipango wa kuacha muziki baada ya ndoa. Kwani sitegemei kama mtoto wangu atanikuta kwenye mashine (kutengeneza muziki). Ila kwa upande wa studio itakuwepo.”