Shareez anatafuta mdhamini wa kutengeneza video ya wimbo wake mpya

0

Rapa kutokea Zanzibar Shareez amesema anatafuta mdhamini kwa ajili ya kutengeneza video ya wimbo wake mpya ‘Umebadilika’ ambao bado hajauachia.

shareez

Akizungumza na Zenji255 Shareez amesema kuwa wimbo upo tayari na amefanya hapa hapa Zanzibar na ameshirikiana msanii kutoka Zambia anaitwa ‘Kasi’ ila ugumu anaoupata ni gharama za kulipia kwenye kutengeneza video.

“Kama kutakuwa na mdhamini yoyote ambaye atakubaliana na gharama zinazoendana na huu wimbo mimi sina tatizo, nitafanya bila ya wasi. Nawakaribisha wadau watakaokuwa wamevutiwa na wazo langu” Alimalizia Shareez.