Ali Yanga, Shabiki namba moja wa Yanga afariki dunia

0

Moja kati Mwanachama aliejizoelea umaarufu mkubwa ndani ya klabu ya soka ya Yanga SC  na nchini kwa ujumla aliyefahamika kwa jina maarufu kama Ali Yanga amefariki dunia.

Katika taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imesema kifo cha shabiki huyo kimeacha pengo kubwa kwa nafasi yake ambayo ilipelekea kujipatia umaarufu mkubwa pamoja na kuwa balozi mzuri kama mwananchama wa timu hiyo.
Marehemu atakumbukwa kutokana na mbwembwe zake alizokuwa akizionesha anapokuwa uwanjani na nje ya uwanja hasa pale timu yake inapokuwa katika mchezo.

Uongozi wa Zenji255.com tunatoa pole kwa wapenzi wa soka Tanzania pamoja na familia yake.