Saida Karoli kurudi tena katika jukwaa la Sauti za Busara 2018

0

Kwa kipindi kirefu tokea mwaka 2005 mwanamuziki Saida Karoli alishiriki katika Tamasha la Sauti za Busara ambalo litaruka katika anga za Afrika mnamo tarehe 8 Februari, katika viwanja vya Ngome Kongwe Zanzibar.

saida karoli

Mwanamuziki huyo amesema kuwa ni muda mrefu hajafanya maonyesho yake katika visiwa vya Zanzibar kutokana na kuamua kupumzika kimuziki na kuangalia hali ya hewa inaendaje katika soko la muziki hapa Tanzania.

“Ni miaka 15 sasa tokea nifanye Sauti za Busara nifanye onyesho langu la mwisho katika tamasha hilo na mwaka huu narudi tena. Nikiwa na mirindimo yangu ya¬† zamani ni mipya, ikiwemo chambua kama karanga ambayo ilinipa jina kubwa la kuwa mwanamuziki bora wa nyimbo za asili” Amesema Saida Karoli.

Tamasha la Sauti za Busara linatarajiwa kuanza mwezi wa Februari 8 – 11, ambapo watakuwepo wasanii kutoka nchi mbali mbali za Afrika.