Said Fella asema ana ndoto za kugombania urais 2040

0

Meneja wa kundi la kukuza vipaji la Mkubwa na Wanawe, Said Fella amesema ana ndoto za kugombania uraisi ifikapo 2040.

said fella

Akiongea na Zenji255 Fella amesema kuwa katika maisha ni lazima uwe na malengo na kumtanguliza mungu akusaidie katika malengo na mipango yako yafanikiwe.

“Kila mtu anaishi na ndoto na hakuna mtu aliyezaliwa na mama yake halafu hapo hapo akaambiwa kwamba atakuwa mtu mwenye cheo kikubwa duniani. Kwahiyo ndoto zangu nikizifanyia kweli nina imani mungu atakuwa na mimi na atanisaidia juu ya mipango yangu ya maisha.” Amesema Said Fella