Rohan Marley na Lauryn Hill wapata mjukuu kutoka mtoto wao Zion

0

Lauryn Hill na mtoto wa mwanamuziki Bob Marley, Rohan Marley watakuwa wanaitwa bibi na babu kuanzia sasa, baada ya mtoto wao wa kwanza wa kiume Zion wikiendi hii kupata mtoto.

lauryn hill

Baba wa Zion Rohan Marley, ambaye aliyezaa na Lauryn Hill watoto watano, ametoa taarifa hiyo kupitia mtandao wa Twitter, huku akiwa amemshikilia mjukuu wake anaeitwa Zephania Nesta Marley. “JAH BLESSINGS ‘WE GIVE THANKS FOR LIFE Welcome to Earth Little ZEPHANIAH NESTA,” aliandika Rohan kupitia Twitter (Feb. 19)

https://twitter.com/Romarley/status/833531122944450560

Hata hivyo kwa upande wa Lauryn Hill hakuonekana kutoa taarifa yoyote kuhusiana na ujio wa mjukuu wake huyo Zephania.

Hongera kwa Zion