Rico Single asema ‘Zanzibar hakuna watu wenye pesa na kujitolea kwenye muziki’

0

Msanii mkongwe wa Zenji Fleva Rico Single amesetoa sababu inayofanya mziki wa zanzibar kusuasua ni kutokana kuwa hamna makampuni yanayoweza kufanya kazi na wasanii hapa Zanzibar.

rico

Akizungumza na Zenji255 Rico Hivi karibuni alitambulisha wimbo wake mpya ‘Yani Raha’ ambao wenye mahadhi tofauti ambayo yaliyozoeleka katika nyimbo zake alisema kuwa “kwa hapa kwetu hamna watu wenye pesa ambao wanapenda muziki hiyo ndio sababu kubwa inayofanya mziki wetu kusogea kwa taratibu utaona msanii anapeleka nyimbo radio anafanya promo mwenyewe anatafuta show yaani kila kitu anafanya mwenyewe hili ni tatizo.”

Lakini pia Rico amesema ana imani kuwa ipo siku muziki wa Zanzibar utakuja kueleweka na utapata wafadhili kutoka kila sehemu na kupata ushabiki wa hali ya juu kabisa.