(Video): Real Madrid Kukutana na Atletico Madrid Fainal za UEFA Baada ya kuifunga Man City 1-0

0
madrid

Nusu fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imechezwa Usiku wa May 4 2016 kwa klabu ya Real Madrid ya Hispania, kuwakaribisha Man City ya Uingereza katika nusu fainali ya pili iliyochezwa uwanja wa Santiago Bernabeu. Real Madrid imefanikiwa kutinga fainali kwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

Mchezo wa kwanza uliochezwa wiki iliyopita Real Madrid walicheza ugenini katika uwanja wa Man City uitwao Etihad na mchezo kumalizika kwa sare ya kutofungana, lakini Real Madrid walicheza bila mchezaji wao nyota Cristiano Ronaldo ambaye mchezo wa leo alikuwepo. Goli pekee la Real limepatikana kwa Fernando  kujifunga dakika ya 20.

Real Madrid wamewahi kufungwa na timu mbili kutoka Uingereza ambazo ni Arsenal na Liverpool katika uwanja wa  Bernabeu 2006 na 2009. Kwa sasa Real Madrid imefikisha jumla ya mechi 15 ilizocheza Bernabeu dhidi ya vilabu vya Uingereza, imefungwa mara 2, sare mara 5 na wameshinda mara 8