Rayvanny aelezea ‘Salome’ imempa umaarufu mara mbili

0

Rayvanny, msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye ameshirikishwa kwenye wimbo wa Salome na Diamond Platnumz, amesema ‘kolabo’ yake ya wimbo wa salome aliyoshirikishwa na Diamond Platnumz umempa umaarufu na mafanikio zaidi.

rayvanny

Ray amesema wimbo huo umemfungulia milango mingi ya kufanya show hadi nje ya nchi ikiwemo China na Marekani.

Akiongea na eNewz Ray amesema “Wimbo huo umeniongezea show za nje nyingi na kolabo nyingi na wasanii wa nje ambazo watu watazisikia siku si nyingi lakini pia wimbo huo umeniongezea umaarufu sana katika jamii umaarufu niliokuwa nao mwanzo umekuwa mara mbili zaidi” alimalizia hivyo Ray.

Lakini pia Ray amesema wimbo huo wa salome haukuwa na lengo la kuzima wimbo wa msanii yeyote kwa kuwa kila mtu ana njia zake na mashabiki zake huku akiamini kuwa watu wanaoweza kuzima wimbo wa mtu ni watangazaji au vituo vya radio lakini pia Ray hakusita kumsifia Diamond huku akisema ni mtu mwenye roho ya kipekee sana.