Rais Dk. Shein asema serikali imejidhatiti kuendeleza mapinduzi ya ilimo

0

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema serikali imejidhatiti kuendeleza kwa vitendo Mapinduzi ya Kilimo kwa kuwapa taaluma ya kilimo bora wakulima, wafugaji na wavuvi, pamoja na kuendeleza huduma za ugani.


Dk. Shein amesema hayo katika ufunguzi wa Maonesho ya siku ya chakula Duniani, yaliofanyika katika viwanja vya Chamanangwe, Mkoa Wa Kaskazini Pemba.
Amesema Serikali inaendelea kuweka mazingira mazuri ya kibiashara ili kuwawezesha wafanyabiashara kuingiza na kuuza zana, vifaa na pembejeo za kisasa kwa wakulima kwa urahisi.
Aidha, Dk. Shein amesisitiza haja ya wakulima kulima kwa kuzingatia matumizi ya mbinu za kisasa za kilimo pamoja na kufuata maelekezo ya wataalamu.
Aidha, amewataka Wakuu wa Wilaya kote nchini kuongeza kasi ya mashirkiano na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, sambamba na kusimamaia ipasavyo maendeleo ya kilimo katika Wilaya zao.


Mapema, Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Mmanga Mjengo Mjawiri, amesema Wizara hiyo kwamashirikiano na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imejidhatiti kuendelea kutoa elimu kwa wananchi katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi juu ya lishe bora pamoja na matumizi endelevu ya rasilimali zilizopo, sambamba na kuwataka wananchi, hususan vijana kutumia maonesho hayo kupata ujuzi.