‘Q Chillah angenifunika, wimbo nisingeupeleka radio’ – Triple M

0

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Zanzibar Mansour Malik ‘Triple M’, amesema katika wimbo wake aliomshirikisha Q Chillah ‘Tobo la Pili’ asingeupeleka radio kutokana na madai ya kufunikwa katika wimbo huo.

triple m

Alifunguka hayo ijumaa hii wakati alipokua katika mahojiano na Zenji255 “unajua wakati natengeneza ngoma yangu ya tobo la pili Q Chillah alikuepo pembeni kwahiyo aliposikia melody akapenda akaniomba aingize vocal zake kwahiyo ikawa rahisi sana kufanya nae kazi nashukuru mungu ngoma ilinitambulisha vizuri kwa Zanzibar na bara pia.”

Triple M kwa upande mwingine¬† amezungumzia kuhusiana na muziki wa Zanzibar na ushindani wa maproducer bado ni mdogo sana, alisema ni ngumu kumpata producer anaeweza kushindana na maproducer wa kubwa wa tanzania bara. “sina chuki na producer yoyote hapa zanzibar ukweli ni kwamba maproducer wetu wanahitaji kujituma zaidi kwanini nyimbo anazofanya aloneym zikienda hazirudi lakini za maproducer wengine nyimbo zao zinarudi hapo inatakiwa wakae chini wajiulize sehemu gani wanapokosea.” Alimalizia Triple M.