‘Producers wengi wa bongo hawana tofauti kabisa na wabeba mizigo’ – Hermy B

0

Mtayarishaji wa muziki na mmiliki wa studio ya ‘B Hits’ Hermy B amefunguka na kusema kuwa watayarishaji wengi wa muziki nchini Tanzania ni masikini na maisha yao hayafanani kabisaa na majina yao.

hermy b

Hermy B amesema hayo kupitia account yake ya twitter na kudai kuwa watayarishaji wengi wa muziki wa bongo hawana tofauti na watu wanaobeba mizigo (Makuli) kwani wanafanya kazi kubwa sana lakini kipato wanachopata kutokana na kazi hiyo ni kidogo mno kiasi cha wengi kuwa na maisha ya chini ukilinganisha na majina yao.

Lakini mbali na hilo Hermy B alisema kuwa hana uhakika kama baadhi ya wasanii wa bongo wanakumbuka kufanya Investement ili kuzidi kujiongezea kipato kutokana na pesa ambazo wamekuwa wakipata kupitia muziki wao na dili za hapa na pale.