Producer Bonge Jr. kumrudisha N.I kwenye ‘game’

0

Mtayarishaji kutoka studio za Melanin Media Producer Bonge Jr. amesema ana mipango ya kumrudisha msanii aliyekuwa akiunda kundi la BZ Broo (Brooklyn) N.I katika muziki.

bonge

Akizungumza na Zenji255 Bonge amesema kuwa kuna wasanii wengi wa hapa Zanzibar alikuwa anatamani kufanya nao kazi na N.I alikuwa ni mmoja wapo.

“Msanii kama N.I kwanza uwezo wake ni mkubwa toka zamani jamaa (N.I) nilikuwa nampenda sana jinsi anavyocheza na melody za muziki. Na uzuri wa N.I muda wowote ukikutana nae ni muelewa na ninaelewa kwamba matatizo yote aliyoyapata ni stress za maisha na muziki wake hapo mwanzo”

Kwa upande mwingine Bonge amesema kuwa tayari kazi zake zishaisha na awaahidi mashabiki wa N.I kuwa karibuni atasikika hewani.