Producer Bab Chidy azungumzia ujio wa studio ya Moss Wanted na Wrong turn

0

Mtayarishaji wa muziki wa kizazi kipya Bab Chidy amezungumzia kuhusiana na ujio mpya wa studio ya Moss Wanted ambayo studio hiyo mmiliki wake ni ndugu wa msanii Bodea.

bab chidy

Akizungumza na Zenji255 Bab Chidy amesema studio itakuwa ikishirikiana na wasanii wa Zanzibar katika tasnia tofauti kwani sio muziki peke yake hadi video watakuwa wakifanya.

“Kampuni yetu ni mpya na malengo yetu ni kufanya mapinduzi katika muziki wa Zanzibar na kuna kazi kama za wrong turn ambayo kila kitu chao kipo tayari na kwa Tanzania bara kuna kazi ya Mo Rocka ambaye hivi sasa tayari kishaondoka kwani alikuwepo kwa siku tatu hapa Zanzibar” Amesema Bab Chidy