Pozi Adimu uso kwa uso na Shilole

0
pozi

 

Msanii mkongwe katika gemu ya muziki wa kizazi kipya Zanzibar, ambaye kwa aasa anafanya vizuri na Ngoma yake ya MsobeMsobe, amekutana na mwanadada Shishi baby (Shilole) Ndani ya jiji la Dar es salaam.

Pozi adimu alisema ameenda dar kwa ajili ya interview aliyoitwa na kituo cha Tv cha ITV kweny kipindi maarufu cha THE BASE, kinachoruka hewani Jumatatu hadi Ijumaa saa 11 jioni.

Kuhusu makutano yake yeye na mwanadada Shilole, Pozi alikataa kusema chochote huku akisema watu wasubirie tuu, km kuna kitu watajua muda ukifika.  Pozi aliweza kuzungumzia kuhusiana ‘collabo’ na mwanadada huyo. “Unajua sio kila msanii ukikutana nae kuna kua na collabo tuu, yapo mambo mengi ambayo yanaweza kusaidia mziki wako kupenya kwao, Mimi na Shilole kuna vitu tumeongea kwa pamoja na mambo amabayo yataleta tija kwenye Mziki wetu wa Zanzibar, Mashabiki wasubirie Watajua wakati ukifika”