Picha: Ufunguzi wa Tamasha la ZIFF 2017

0

Siku ya Jumamosi tarehe 8 Julai, ilikuwa ni siku ya kutimiza miaka 20 ya Tamasha la Filamu za nchi za majahazi Zanzibar (ZIFF) ambapo ufunguzi wake ulifanyika katika ukumbi wa Ngome Kongwe.

katika ufunguzi huo kulihudhuriwa na wageni kutoka nchi mbali mbali ambapo mgeni rasmi katika tamasha hilo alikuwa ni raisi mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe Jakaya Mrisho Kikwete.

Baada ya ufunguzi wa Tamasha, filamu ya T-Junction ndio ilikuwa ya kwanza kuonyeshwa ambayo iliyotengenezwa na waongozaji kutoka Tanzania kama Amil Shivji na wengineo.

Kauli mbiu ya tamasha hilo Kujisiki furaha ambalo litaendelea mpaka tarehe 16 Julai.

Angalia picha za ufunguzi huo.