Picha: Tamasha la kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera

0

Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva wameibuka washindi kwa penati tano kwa nne dhidi ya wasanii wa Bongo Movie katika mechi ya hisani kwa ajili ya kuwachangia waathirika wa tetemeko la ardhi Bukoba.

Katika mechi hiyo iliyofanyika uwanja wa Taifa ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, ambayo ilikuwa na ushabiki mkubwa kwani wasanii wa Bongo fleva waliungana na wasanii kutoka Zanzibar na kuweza kufanya timu yao kuibuka na ushindi wa penalti 5 kwa 4. Awali hapo mwanzo mechi hiyo ilimaliza 1-1 ambapo goli la Bongo Movie lilifungwa na Mteze na H.Baba dakika chache baadae akasawazisha.

Katika mechi nyingine kati ya wabunge wa Yanga na wabunge wa Simba, wabunge wa Yanga waliondoka na ushindi baada ya kuwafunga wabunge wa Simba goli 5 kwa 2.

Angalia picha za matukio mbalimbali.

img_7906 img_7907 img_7933 img_7942 img_7950 img_7951 img_7954 img_7980 img_7982 img_8000 img_8002 img_8014 img_8015 img_8030 img_8032 img_8035 img_8038 img_8042 img_8047 img_8063 img_8075 img_8079 img_8087 img_8094 img_8096 img_8119 img_8131 img_8177 img_8184 img_8194 img_8266 img_8286