Picha: Taifa jang’ombe washinda 2-0 dhidi ya Jang’ombe Boyz

0

Timu ya Taifa Jangombe usiku wa Novemba 19 waliwafunga mahasimu wao Jang’ombe Boyz goli 2-0 katika uwanja wa Amani Zanzibar.

taifa

Wachezaji Mohd Said Mohammed aliyefunga goli la kwanza dk’ 14 ambapo goli la pili lilifungwa na Baraka Ushindi Manaman dk’ 86.

Licha ya Jang’ombe Boys jana kufungwa 2-0 na Taifa Jang’ombe lakini katika Historia ya timu hizo mbili walishacheza michezo mitatu ambayo waliokutana kati ya Jang’ombe Boys na Taifa Jang’ombe na Jang’ombe Boys walishinda mara mbili na Taifa wameshinda moja.

Timu hizo zitakutana katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja siku ya Jumamosi disemba 10 saa 10:00 za jioni katika Uwanja wa Amani ambapo huo utakuwa ni mchezo wa nne kukutana wawili hao.

4 1 3

Picha zote na Abou Kisandu