Picha: Rahatul-Zaman na Smile walivyotoa burudani katika uzinduzi wa ‘The Dream’

1

Usiku wa jana (Jan. 28) kikundi cha taarab asili cha Rahatul-Zaman na msanii wa kizazi kipya Smile, walitoa burudani katika uzinduzi wa filamu mpya ya ‘The Dream’ katika ukumbi wa Ngome Kongwe Zanzibar.

Hii ni mara ya kwanza kwa tasnia ya filamu hapa visiwani kufanyika uzinduzi kama huu ambapo mgeni rasmi wa usiku huo alikuwa mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Ayoub Mohammed na walihudhuria wageni mbali mbali akiwemo mwakilishi wa jimbo la Kikwajuni Al-Jazeera.

Katika uzinduzi kulikuwa na ugawaji wa vyeti kwa wadhamini mbali mbali waliosaidia kufanikisha filamu hiyo mpaka ikakamilika vile vile kulifanyika mnada wa kuiuza CD ya filamu hiyo pamoja na vikombe na pia Mkuu wa mkoa alipatiwa zawadi ya vibuli kutoka Rwanda.

Angalia picha za uzinduzi huo hapo chini