Picha: PBZ wafungwa 1-0 na Z.F.U katika mechi ya hisani Uwanja wa Amani, Zanzibar

0
pbz

Timu ya wasani wa muziki wa kizazi kipya Zanzibar (ZFU) jana iliwafunga timu ya wafanyakazi wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ goli 1-0 katika mechi ya hisani ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Wananchi waliopata maafa ya mvua na wahanga wa kipindupindu.

Goli la kwanza la timu ya wasanii wa kizazi kipya lilipatikana katika kipindi cha kwanza kwenye dakika 30 na mfungaji alikuwa Mbwana (MB Doctor) lakini wakati akifunga goli hilo mchezaji ilimlazimu atoke nje baada ya kugongana na goli kipa na kuumia mguu.

Katika mechi hiyo kulipambwa na burudani mbali mbali, wasani kama Pozi Adim, Abramy, Jakaya, na Dancers wa Benefit 7 waliweza kuzifurahisha nyoyo za watizamaji waliokuwepo katika mechi hiyo.

Mgeni rasmi aliyealikwa katika mechi alikuwa ni waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma na mke wa Makamu wa pili wa Rais mama Asha Balozi. mechi hiyo iliweza kuchangisha shilingi Milioni 7 ambapo Benki ya Watu wa Zanzibar ilichangia shilingi milioni 5 na mchango uliochangishwa uwanjani papo hapo ulifanikiwa kufika hadi shilingi milioni 2.

DSC_0371 DSC_0393 IMG_3987 IMG_3996 DSC_0399 IMG_2896 IMG_2887 IMG_2885 IMG_2878

_MG_3970

DSC_0423 IMG_2876 IMG_3978 IMG_4006

 

DSC_0364 DSC_0365 DSC_0381

Picha na Othman Mapara