Picha: Nokia 3310 imerudi na muundo mpya

0

Je ulishawahi tumia simu ya Nokia 3310? Na unaukumbuka muundo wake ulivyokuwa? Basi imezinduliwa tena rasmi baada ya miaka 17.

Wengi wanaiona simu hiyo kuwa nzuri kutokana na umaarufu wake na uthabiti.Zaidi ya simu milioni 126 zilitengezwa kabla ya kuondolewa katika soko 2005.

Simu mpya iliokarabatiwa itauzwa chini ya leseni ya kampuni ya Finland ya HMD Global ambayo pia ilizindua simu kadhaa za Nokia aina ya smartphone.

Mtaalam mmoja alisema ni njia nzuri ya kuzindua simu za Nokia.

”Simu hiyo ya 3310 ilikuwa ya kwanza katika soko na inasubiriwa na wengi” ,alisema Ben Wood, mshauri wa kiteknolojia.

”Hatua hiyo ya kuzindua upya Simu ya 3310 ni wazo zuri na tunataraji itauza kwa wingi”.

Source: BBC Swahili