Picha: Mazishi ya Muimbaji Fauzia Abdallah

0
Mwimbaji gwiji wa muziki wa TAARAB asilia kutoka Zanzibar wa kundi maarufu duniani lenye miaka zaidi ya 105 Nadii Ikhwaan Safaa (Malindi Musical Club), Bi Fauzia Abdallah, Jana May 12 alipelekwa kupumzishwa kwenye makazi yake ya milele katika makaburi ya Mwanakwerewe, Zanzibar.
Bi Fauzia amefariki dunia hospitali ya Muhimbili alfajiri, Mei 11 akiwa katika wodi ya Kibasila alikokuwa akipata matibabu ya saratani. Marehemu alitamba sana katika miaka ya 1980 akiwa na kundi hilo la Malindi Musical Taraab na nyimbo zake nyingi “Lishalo Limekwisha” na “Nimesalitika”.
Pia bi Fauzia alikuwa mke wa mtunzi mahiri na mpiga qanoun Ally Salum Bassallama wa kundi hilo maarufu ambalo ndilo kundi la mwanzo la taarab barani Afrika lililoanzishwa mwaka 1905 huko Zanzibar.
Marehemu Bi Fauzi ameacha watoto watatu. Mola amlaze mahala pema peponi amen.

Source: Saluti5
f1 f3 f4 f5 f6 f7
Picha na Zanzibar24