Picha: Kupokelewa na Kuzikwa kwa mwili wa Marehemu Aboud Jumbe

0

Mwili wa aliyekuwa Raisi wa awamu ya pili Zanzibar, Marehemu Aboud Jumbe amezikwa jumatatu Agosti 15 visiwani Zanzibar nyumbani kwake Migombani.

Viongozi mbali mbali walihudhuria katika mazishi hayo akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Ali Mohammed Shein.

Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi alishika wadhifa wa Rais wa Zanzibar April 7, 1972 mara baada ya kifo cha aliyekuwa rais wa kwanza wa Zanzibar Abeid Amani Karume.

Hayati Aboud Jumbe alijiuzulu urais wa Zanzibar pamoja na nyadhifa nyingine za makamu mwenyekiti wa CCM na makamu rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Januari 30, 1984.

Marehemu amefariki akiwa na umri wa miaka 96 ameacha watoto 13, na wajukuu 40, Mwenyezi ailaze roho ya marehemu popeni Amina.

1 3 4 5 6 8 9 10 11 12 14