Picha: Ison Mistari ashoot video ya ‘Nani Nilimkosea’

0

Rapa ambaye kwa hivi sasa anasimamiwa na lebo ya Stone Town Records, Ison Mistari hivi karibuni alionekana akishoot video ya wimbo wake mpya ‘Nani Nilimkosea’ huku akiwa na timu yake nzima ya lebo hiyo.

ison

Akizungumza na Zenji255 leo Ison alisema kuwa video imesimamiwa na watayarishaji wawili Abdul (TZ) na Guitoast (GER).

“Video mpaka hivi sasa maandalizi ya mwanzo yote yashakwisha, Naishukuru timu yangu nzima kwa kufanikisha hili jambo.” amesema. “Video tumeifanyia Zanzibar na maeneo tuliyotumia kwa ajili ya video ni tofautina watu watashangaa jinsi ya mandhari ya video yenyewe, Kwani tumefanya katika mitaa ya Stone Town, chuo cha muziki DCMA na katika kisiwa cha Funguni (SandBank). Kwahiyo ninachowaomba watu wetu wakae mkao wa kula na kuupokea ujio mpya wa video.” Alimalizia Ison Mistari.

Angalia picha za shuhuli hiyo katika maeneo tofauti

img_0231 _mg_0097 _mg_0116 _mg_0159 _mg_0206 _mg_0223 _mg_0268 _mg_0301 _mg_0358 _mg_0430