Picha: Harakati za mwezi wa Ramadhani katika soko kuu la Mwanakwereke, Zanzibar

0

Wakati tukiwa katika kumi la mwanzo la mwezi mtukufu wa Ramadhani, wananchi huwa katika pirika pirika za kutafuta mahitaji yao ya vyakula kwa ajili ya futari. Zenji255 ilipita katika soko la Mwanakwereke, Zanzibar nakuona harakati za wananchi wakijipatia futari katika Soko Kuu hilo.

1Bei za vyakula vya nafaka katika Soko Kuu la Mwanakwerekwe Mjini Unguja leo kama inavyoonekana pichani.

2Bei ya Nazi katika soko la mwanakwerekwe bei ya jumla inategemeana na ukubwa wa nazi zimeanzia na bei ya shilingi 400/= na 500/= katika soko la jumla sokoni hapo na bei ya rejareja inaizwa shilindi 550/= na 700/=

3 4Mjasiriamali katika Soko la Mwanakwerekwe akipanga viazi vitamu fungu moja la viazi vitamu ni shilingi 2000/= na 5000/=

5 6Wananchi wakipata futari ya majimbi katika Soko Kuu la Mwanakwerekwe Unguja fungu mmoja la majimbi katika soko hilo linauzwa kati ya shilingi 2000/= na 5000/= kwa fungu moja.

Picha zote kwa hisani ya: Zanzinews