Picha: Everton kupambana na mshindi wa michuano ya Sports Pesa Julai 13

0

SportPesa imeanza kuthibitisha nia yake ya kendeleza soka la Tanzania kwa kutangaza kuwa mshindi wa michuano ya SportPesa Super Cup atawavaa miamba wa soka wa Uingereza, Everton. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa klabu ya Ligi Kuu ya England kucheza na klabu ya soka ya Afrika Mashariki.

Sports Pesa

Tangazo hil limetolewa katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika wenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam uliohudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SportPesa, Pavel Slavkov, Mkurugenzi wa Utawala wa SportPesa, Tarimba Abbas, Muu wa masoko wa Kimataifa, Joyce Kibe, Mkurugenzi Mtendaji wa Everton, Robert Elstone, Balozi wa Everton FC, Leon Osman, Waziri wa Michezo Dk. Harrison Mwakyembe, Mkurugenzi wa Michezo Yusuph Singo, Rais wa TFF Jamal Malinzi na wanahabari. Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu itapigwa Julai 13 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, (kushoto) kizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Everton Robert Elstone, wakati wa hafla hiyoiliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

SportPesa ilitangaza Mei 24 kwamba michuano ya SportPesa Super Cup itafanyika jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Uhuru ikishirikisha timu nne (4) za Tanzania dhidi ya timu nne (4) kutoka Kenya. Timu sita (6) kati yazitakazoshiriki michuano hiyo ni klabu washirika rasmi wa SportPesa. Simba SC, Young Africans SC na Singida United FC ni washirika wa SportPesa Tanzania wakati Nakuru All Stars, AFC Leopards na Gor Mahia ni washirika wa SportPesa kutoka Kenya. Tusker FC ndio mabingwa wa Ligi Kuu ya SportPesa ya Kenya wakati Jang’ombe Boys FC ni vinara katika Ligi Kuu ya Zanzibar.

Mchezaji wa zamani wa timu ya Everton, Leon Osman (kushoto) akimfurahia na kumpigia makofi,kijanaAbubakar Said wa Kituo cha michezo cha Wakati ujao wakati wa Kliniki iliyofanyika Uwanja wa Taifa
Mchezaji wa zamani wa timu ya Everton, Leon Osman, akisalimiana na mchezaji wa timu ya Kituo cha michezo cha Wakati Ujao Duce, Ezekiel Msuva ambaye ni mdogo wa mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania,Simon Msuva, wakati mchezaji huyo alipowatembelea katika Kliniki yao Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo Juni 1, 2017. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe.
Mchezaji wa zamani wa timu ya Everton, Leon Osman, akisalimiana na mchezaji wa timu ya Kituo cha michezo cha Symbion cha JK Yourth, na timu ya Taifa ya Vijana chini ya Umri wa miaka 17, Serengeti Boys, Lenox Musombo, wakati mchezaji huyo alipowatembelea katika Kliniki yao Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo Juni 1, 2017. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Everton Robert Elstone
Mtoto Hamis Kassim wa Kituo cha michezo cha Bom Bom, akionyesha umahiri wake wa kuchezea mpira wakati wa hafla hiyo ya Kliniki
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, (wa Nne kulia) Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo, Mchezaji wa zamani wa timu ya Everton, Leon Osman (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Montage Ltd, Teddy Mapunda, wakipita kukagua timu za vijana za Academy, wakati wa Kliniki ya kuwahamasisha katika mchezo wa Soka katika hafla iliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam