Picha: DJ Waiz ashoot video ya ‘Shobo Robo’

0

Hatimaye msanii na mwanamitindo wa muda mrefu, DJ Waiz ameshoot video ya wimbo wake mpya ‘Shobo Robo’ ambayo alioshirikiana na Baby Jay na Kijukuu.

Akiongea na Zenji255, Waiz amesema kuwa kwa kipindi kirefu alikaa kimya ni kutokana na majukumu ya mitindo kuwa mengi na kwa upande wa muziki ilimbidi ayasome mabadiliko yaliyokuwepo katika muziki ili ajue anarudi kwa ‘style’ gani.

“Muziki kiukweli umekuwa hivi sasa kwa hapa kwetu, vijana sasa hivi wameamka sana kimuziki na ndio maana nikaamua nirudi kwa presha ya hali ya juu kuanzia wimbo mpaka video” Amesema DJ Waiz.

Video ya wimbo huo imetayarishwa na Director Pablo na imetumika siku tatu kuitengeneza video hiyo, na katika video wanamitindo mbali mbali walishirikishwa akiwemo Chidy Adore na wengine wengi. Video inatarajiwa kuachiwa wiki moja kuanzia sasa.

Picha kwa msaada: Chiwile Jr.