Picha: DJ Khaled anunua jumba la kifahari la Beverly Hills $9.9 Milioni

0

Msanii kutokea nchini Marekani, DJ Khaled ameinunua nyumba ya kifahari ya Beverly Hills iliyokuwa ikimilikiwa na muimbaji na muigizaji maarufu Robbie Williams kwa dola millioni 9.9za kimarekani, Kwa mujibu wa mtandao wa Variety.

Nyumba hiyo ya kifahari ilimilikiwa na Robbie toka mwaka 2002 ambapo aliinunua kutoka kwa mwanamuziki wa miondoko ya Country Clint Black na muigizaji wa kike Lisa Hartman kwa dola Million 5.45.

Angalia picha za nyumba hiyo ya kifahari kwa ndani